Mwenyekiti wa Mawakala Wazawa wa Utalii Tanzania (TLTO) Bw. Samuel Diah ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuahakikisha kuwa wanawakumbusha na kuwahimiza wanachama wao kulipa kodi kwa wakati.
Bw. Diah ameyasema hayo leo tarehe 08.06.2025 alipotembelewa na Meneja wa TRA Mkoa wa Arusha Bw. Deogratius Shuma katika maonesho ya ya utalii ya Karibu-Kilifair2025 yaliyomalizika leo jijini Arusha.
Bw. Diah ameelezea kuwa kutokana mahusiano mazuri kati yao na TRA sambamba TRA kuwapatia elimu ya kodi mara kwa mara imesadia sana kuondosha changamoto zao na kuwafanya wahisi kuwa TRA ni kama nyumbani.
“Tumeona sasa hivi kuna urahisi mzuri sana wa kukaa na kuongea, mpango huo umesaidia sana hata wale waliokuwa wanaogopa kufika ofisi za TRA, sasa hivi TRA wameona kama nyumbani kwao.”
Nae Bw. Shuma amewasisitiza kuwa wataendelea kuboresha mahusiano na kuwakumbusha kulipa kodi zao mapema badala ya kusubiri siku za mwisho.