Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akijibu maswali mbalimbali ya wabunge bungeni jijini Dodoma leo tarehe 12 Juni 2025.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akijibu maswali mbalimbali ya wabunge bungeni jijini Dodoma leo tarehe 12 Juni 2025.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akijibu maswali mbalimbali ya wabunge bungeni jijini Dodoma leo tarehe 12 Juni 2025.
….
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis amesema Mradi wa kufua Umeme wa Bwawa wa Julius Nyerere uliopo Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani wenye uwezo wa kuzalisha megawati 2115 unatarajiwa kuchochea matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Amesema hayo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Donge Mhe. Soud Mohammed Jumah aliyetaka kufahamu ni kwa kiasi gani mradi huo umechangia matumizi ya nishati safi ya kupikia na kuepuka ukataji wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa.
Akiendelea kujibu swali hilo Naibu Waziri Khamis amesema tayari Serikali imesambaza huduma ya umeme wa uhakika mijini na vijijini hatua itakachagiza matumizi ya nishati safi ya umeme na kuacha kutumia kuni na mkaa.
Aidha, Mhe. Khamis alisema katika kuimarisha uhifadhi wa mazingira hususan katika maeneo yanayozunguka mradi huo wa kufua umeme, Serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kuhamasisha na kuratibu upandaji wa miti kwenye vyanzo vya maji na kuitunza.
Alisema Serikali imeendelea kutoa elimu ya mazingira, kusimamia utekelezaji wa Muongozo wa Taifa wa Matumizi endelevu ya Ardhi Eneo la Hifadhi ya Mita Sitini kutoka kwenye vyanzo vya maji pamoja na kuunda Kamati za Mazingira kwa ajili ya kudhibiti uharibifu wa mazingira kwenye vyanzo vya maji.
Alisema hayo wakati akijibu swali la msingi la Mhe. Soud aliyeuliza kuna mkakati gani wa kuimarisha uhifadhi wa mazingira ya Mradi wa Bwawa la Nyerere ili kuhakikisha uendelevu wa mradi.
“Ushirikishwa wa wananchi waishio karibu na mradi huo unafanyika wa kiasi kikubwa na tumewapa jukumu la kutunza mradi na pia tunawahimiza kupanda miti ambayo haikaushi maji, vilevile tunashirikiana na maafisa wa mazingira na mabalozi wa mazingira, lakini pia tunawahamisha mara kwa mara wafanye usafi ili eneo la bwawa liendelee kuwa safi,“ alisema.
Kwa upande mwingine, alisema Serikali itaendelea kuwachukulia hatua wanaojihusisha na vitendo vya ukataji miti hususan maeneo yanayozunguka miradi mikubwa na vivutio vya utalii hususan Mlima Kilimanjaro.
Alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mbunge wa Moshi Vijijini Prof. Patrick Ndakidemi kuhusu hatua gani Serikali inawachukulia hatua wanaokata miti katika hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.
Itakumbukwa kuwa Mradi wa Bwawa la Nyerere unalenga kufikia malengo ya Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024 – 2034) kuwa asilimia 80 ya Watanzania kuhamia kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Hivyo, hizo ni juhudi za Serikali chini ya Rais Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amewa kinara katika kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia.