
Na Oscar Assenga,MUHEZA
MWENGE wa Uhuru unatarajiwa kuwasili katika wilaya ya Muheza Ijumaa June 13 ukitokea wilaya Korogwe ambapo utazindua miradi 7 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Biloni 1.6 na utakimbizwa kwa umbali wa kilomita 90.4.
Hayo yalisemwa leo na Mkuu wa wilaya ya Muheza Zainabu Abdallah wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema wataupokea mwenge huo ukitokea wilaya Korogwe na ukiwa kweye wilaya hiyo utaweka mawe ya msingi miradi miwili,miradi minne itazinduliwa na mmoja utakaguliwa
Akizungumza maandalizi ya ujio huo wa mwenge mwaka huu alisema kwamba mwaka jana walikuwa namba moja kimkoa wilaya ambapo alisem wamejipanga katika maeneo ya miradi kuhakikisha inakuwa bora na viwango lakini kuhakikisha hamasa ya kutosha inakuwepo eneo la mpokezi,kwenye miradi na mkesha.
Aidha alisema katika mkesha wa mwenge huo wa uhuru watakuwepo wasanii mbalimbali ili kuweza kutoa burudani mbalimbali kwa wakazi wa mji huo na wageni ambao watashiriki huku akitoa wito wajitokeze kwa wingi kwa maana utakuwa wa aina yake kutokana na namna walivyojipanga.
Hata hivyo alisema pia watakuwa na kongamano maalumu la vijana na Mgeni rasmi atakuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji nchjini (TIC) Gilead Teri sambamba na watoa mada mashuhuri na wabobezi .