Wakazi wa kata ya Bunda Stoo katika halmashuri ya Mji wa Bunda Mkoani Mara wamesema wanajivunia maendeleo yalioyopelekwa na serikali katika kipindi cha miaka mine ya Dkt Samia suluhu Hassan ambapo wamepokea miradi yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni tano katika Miradi ya Afya ,Elimu,Maji na Barabara.
Miradi hiyo wamesema nisehemu ya Maeneo ambayo ilikuwa changamoto kubwa wakilinganisha na sasa Mfano katika Sekta ya Afya wakazi hao wamesema walikuwa wanalazimika kutembea umbali wa Takribani km 5 lakini kwa sasa huduma hizo wanapata Maeneo yao ya karibu.
“Zamani unaamka unaumwa unalazimika kwenda DDH hospital nimbali Sana na sisi huku Kupata huduma ilikuwa changamoto sana “Alisema Amosi Juma Mkazi wa Bunda stoo.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Bunda Stoo Flavian Joseph Alisema kutafta Maendeleo haikuwa kazi ndogo kwani kuna Wakati alilazimika kugombana na viongozi wengine ili kuhakikisha fedha zinazoletwa na Serikali zinawafikia Wananchi nahilo lilifanikiwa Kufuatia sasa Miradi mhimu katika Sekta ya Maji ,Elimu ,na Afya imetekelezwa