Na Sophia Kingimali
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ametoa wito kwa Wananchi wa mkoa kujitokeza kupata Msaada wa kisheria katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuanzia juni 16 hadi 25 Mwaka huu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo juni 13,2025 Jijini Dar es Salaam Mkuu wa Mkoa waDar es Salaam Albart Chalamila amesema kuwa Kumekuwa na malalamiko mengi kwa Baadhi ya Wateja wa magari kwenye Maeneo ya Kuuzia Magari Kuuziwa Magari Mabovu.
“Hata kama Shauri Hilo umelipeleka Mahakamani Njoo na Nyaraka, kwenye Ofisi yangu Wapo Watalamu wa Masuala ya kisheria watakusaidia “Amesema Chalamila.
Chalamila Ameongeza kuwa pia waliouziwa Magari Mabovu kwenye Maeneo ya Kuuziwa Magari pamoja na wenye migogoro ya ardhi wanapaswa kuwasilisha Nyaraka Zao ilikuweza kupata Msaada wa kisheria.
“Juni 16 Hadi 25 tutakwenda kwenye Halimashauri zote tukiwa na watalamu wa Sheria na Ardhi ili kutatua Changamoto za kisheria “Aliongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila.
Wananchi wajitokeze kwa wingi kupata huduma za kisheria katika maeneo ambayo huduma hiyo itatolewa katika maeneo mbalimbali katika wilaya
Pia wanaokuja wanapaswa kuja na nyaraka zote zinazopaswa kuwepo ili kusaidiwa kwa haraka na kwa utaratibu mzuri.
Kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia imeanza kutekelezwa mwaka 2023 kwa pande zote za Muungano ambapo Zanzibar ni mikoa mitano na bara mikoa ishirini na sita na kupitia taarifa mbalimbali za vyombo vya habari wananchi zaidi ya milion 4 wamepata huduma ya msaada wa kisheria kupitia kampeni ya Mama Samia.