Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Programu Janja (ALBINO MOBILE APP) ambayo itawezesha kufanya usajili na ukusanyaji wa taarifa za watu wenye ualbino kwa njia ya kidigitali, alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uelewa kuhusu Ualbino yaliyofanyika kwenye uwanja wa Mwanga Center Mjini Kigoma , Juni 13, 2025. Wa pili kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi , Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete , wa pili kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uelewa kuhusu Ualbino yaliyofanyika kwenye uwanja wa Mwanga Center Mjini Kigoma, Juni 13, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya washiriki wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uelewa kuhusu Ualbino wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipozungumza kwa niaba ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye uwanja wa Mwanga Center Mjini Kigoma, Juni 13, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)