Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na mtoto Kassim Majaliwa alipotembelea Kituo cha watoto wenye mahitaji maalum , Sanganigwa cha Kigoma mjini kinachendeshwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Kigoma, Juni 13, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikabidhi msaada wa vyakula kwa Kituo cha watoto wenye mahitaji maalum, Sanganigwa cha Kigoma mjini kinachoendeshwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Kigoma, Juni 13, 2025. Kushoto ni Makamu Baba Askofu Jimbo Katoliki Kigoma Padri Evarist Anthony Guzuye na kulia ni Mkurugenzi wa hicho, Keneth Hageze. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza alipotembelea Kituo cha watoto wenye mahitaji maalum, Sanganigwa cha mjini Kigoma, Juni 13, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza alipotembelea Kituo cha watoto wenye mahitaji maalum, Sanganigwa cha mjini Kigoma, Juni 13, 2025. Kulia ni Makamu Baba Askofu Jimbo Katoliki Kigoma, Padri Evarist Anthony Guzuye na kulia ni Mkurugenzi wa kituo hicho, Keneth Hageze. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Watoto wa kituo cha wenye mahitaji maalum, Sanginigwa cha mjini Kigoma wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipozungumza wakati alipotembelea kituo hicho, Juni 13, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)……….
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Juni 13, 2025 ametembelea kituo cha kulea watoto wenye uhitaji cha Sanganigwa kilichopo mjini Kigoma, kinachosimamiwa na Kanisa Katoliki jimbo la Kigoma.
Akizungumza na watoto na walezi wa kituo hicho, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua mchango wa madhehebu ya dini katika kuwalea kimwili na kiroho watoto wenye mahitaji maalum nchini.
“Kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ninalishukuru kanisa katoliki jimbo la Kigoma, mtu mmoja mmoja na taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa msaada mkubwa kwa Serikali katika kuwalea watoto wetu, hakika mnafanya jambo kubwa na lakumpenda Mungu na wanadamu”
Akisoma taarifa ya kituo hicho kwa Waziri Mkuu, Mkurugenzi wa Kituo hicho Keneth Hageze amesema kuwa kilianzishwa mwaka 1995 na mpaka sasa kimehudumia watoto 1309.
Mheshimiwa Majaliwa alitoa Mchele, Maharage, Mafuta, Sukari pamoja na Taulo za kike.









