Na Mwandishi Wetu
KATIBU wa NEC Oganizesheni na Mafunzo CCM Issa Haji Usi maarufu Gavu amesisitiza Watanzania kuendelea kukiamini Chama cha Mapinduzi kwa kuwa kinaendelea na mipango yake ya kuwaletea Wananchi Maendeleo.
Akizungumza wakati Kongamano la Umoja wa Vijana wa chama hicho UVCCM Wilaya ya Temeke kuelezea utekelezaji wa ilani ya CCM, Gavu amesema kupitia mabadiliko ya Katiba ya chama hicho, yataiwezesha kuisimamia ipasavyo serikali kutekeleza miradi ya kijamii na ile ya kimkakati lengo likiwa ni kuharakisha maendeleo.
Kwa upande wao UVCCM Temeke imekiri kuridhishwa na utekelezaji wa ilani ya CMM 2020/25 huku ukieleza namna Bilioni 900 zilizotolewa ndani ya kipindi cha Serikali ya awamu ya sita ambavyo zimetekeleza changamoto ya madarasa katika vyuo na vyuo vikuu nchini.
Kwa upande wake Zena Mgaya ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Temeke amekemea tabia ya baadhi ya vyama vya upinzani kutweza utu na kufanya vitendo ambavyo vina ashiria uvunjifu wa amani.
Wakati huo huo Ofisa Mipango kutoka Manispaa ya Temeke pamoja na Dk.Siriel Mchembe mlezi wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi vyuo vikuu vya Dar es Salaam wamesema katika miaka minne ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, vyuo vikuu vimenufaika kwa kupata miradi ya ujenzi wa madarasa pamoja na mikopo huku Manispaa ya Temeke ikieleza kupokea zaidi ya Sh.Bilioni 268 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.