Serikali imetumia zaidi ya bil 75 kutekeleza miradi ya maendeleo katika kata ya Mji Mwema na kisha kufanikiwa kupunguza changamoto zilizokuwa zinawatesa wananchi katika sekta ya afya,elimu,barabara,maji na kilimo.
Akizungumza wakati wa mkutano wa kusoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika kata hiyo Nestory Mahenge amesema fedha hizo zimekuwa chachu ya maendeleo kwa wananchi wa Mji Mwema na kisha kuwaomba kuendelea kukiamini na kukipa dhamana ya kuongoza chama cha mapinduzi.
Mahenge amesema katika kipindi cha mwaka 2020/2025 kata ya Mji Mwema imefanikiwa kuongeza shule mbili za msingi na moja ya sekondari na kumaliza kabisa changamoto ya watoto kurundikana darasani na wengine kutembea umbali mrefu kufata elimu.
Katika sekta ya afya amesema serikali imeboresha majengo na vifaa tiba katika zahanati ya kata Mji Mwema pamoja na Uboreshaji wa miundombinu ya barabara ikiwemo barabara ya mitaa wa Nazareth, Lunyanywi, Joshoni na Mpechi ambazo zimejengwa kwa kiwango cha lami.
Baada ya kusikia utekelezaji wa Ilani ambao umefanikiwa kwa kiasi kikubwa lakini mwenyekiti wa CCM Mji Mwema Daud Mlele ambae ni mgeni Rasmi amesema bado suala la ulinzi na usalama ni changamoto kwasababu kumekuwa na matukio mengi ya kialifu.
Kwa upande wao wanachama wa chama cha mapinduzi kata ya Mji Mwema akiwemo Upendo Sixbet na Bosco Msigwa wamesema kwa kiasi kikubwa ahadi za mheshimiwa Diwani zimetimizwa ikiwemo sekta ya Barabara ,afya,elimu na majia kilimo.