Dar es Salaam, Juni, 2025 — Airtel Tanzania, kwa kushirikiana na Infinix Tanzania, imezindua rasmi Infinix NOTE 50 Pro+, ambayo sasa inapatikana katika maduka yote ya Airtel kote nchini. Ushirikiano huu unaleta pamoja kampuni mbili ambazo zote zinatumia teknolojia ya hali ya juu na kutegemewa na watanzania wengi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Infinix NOTE 50 Pro+ uliofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam, Mtaalamu wa Bidhaa wa Infinix Tanzania, Lilian Julius, alieleza kuwa simu hiyo mpya ni ya kisasa zaidi katika matoleo simu za NOTE 50, iliyotengenezwa kwa mtindo unaoendana na maisha ya kisasa na iliyoundwa kwa kuzingatia vijana wa Kitanzania wapenda teknolojia.
“Kifaa hiki ni mchanganyiko kamili wa ubunifu na umaridadi, na baadhi ya vipengele vinavyoifanya kuwa bora zaidi ni pamoja na kipengele kinachoendeshwa na teknolojia ya Akili Mnemba (AI), uwezo wa kuchaji kwa kasi ya juu, na chombo chake cha kudumu na chenye laini cha chuma. Ushirikiano wetu na Airtel Tanzania unakusudia kuimarisha upatikanaji na uwezo mzuri simu ya mkononi nchini Tanzania.” Julius alieleza.
Kwa upande wake, Meneja wa Vifaa vya Intaneti wa Airtel Tanzania, Asnath Mboya, alisema kuwa Infinix NOTE 50 Pro+ ni tumaini jipya ambalo limedhamiriwa kukidhi mahitaji ya wateja wa Airtel kote Tanzania kwa kuwa linatoa kasi na thamani isiyo na kifani, na kuongeza kuwa ushirikiano huo unakamilisha juhudi endelevu za Airtel Tanzania za kukuza uhusiano na wadau mbalimbali katika kwenye tasnia ya teknolojia na ubunifu ili kukuza uwezo wa kutumia simu za mkononi na kuongeza tija.
“Pamoja na uzinduzi wa kifaa hiki cha kubadilisha ushindani kwenye soko la simu za mkononi, tunasaidia kuboresha maisha ya kidijitali kwa wateja wetu kwa kuwawezesha kuwa na simu mahiri ambayo inabadilisha jinsi wanavyowasiliana, kufanya kazi na kufurahia ulimwengu wa kidijitali. Hatua hii inaendana na dhamira yetu ya kuona Watanzania wote wanapata huduma za simu za kidijitali kwa bei nafuu, hivyo kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kidijitali,” alifafanua.
Mboya alieleza zaidi kuwa, “Lengo la uzinduzi huu ni kuwapa vijana na wapenzi wa teknolojia kifaa kinachochanganya ufanisi, akili na mtindo wa kisasa. Kufanya kazi pamoja na Infinix kunahakikisha kwamba simu hii inapatikana kwa mamilioni ya watu kote nchini.”
Vivutio muhimu vya NOTE 50 Pro+ ni pamoja na:
Betri ya 5200mAh yenye uwezo wa kuchaji haraka wa 3.0, ikichajiwai kamili kwa dakika 38 pekee.
Uzoefu wa hali ya juu wa One-Tap AI unaoendeshwa kwa usaidizi wa mfumo wa Akili Mnemba uitwao ‘Folax AI’ kwa ajili ya kutafsiri bila data, utambuzi wa maudhui na usaidizi wa wakati halisi.
Kamera ya 100X Periscope na lenzi ya mbele ya 50MP pamoja na sensa ya SONY IMX896 kwa upigaji picha wa hali ya juu, hata nyakati za usiku.
Utendaji ulioimarishwa wa mchezo kwa kutumia chipu ya MediaTek Dimensity 8350 Ultimate, XBOOST AI ya Michezo, na uoanifu wa mtandao wa 5.5 G.
Mwonekano wa nje ya simu umtengenezwa na ArmorAlloy wenye alumini ya kiwango cha anga na mfumo wa ShockAbsorb kwa uimara na kubebeka usio na kifani.
Infinix NOTE 50 Pro+ sasa inapatikana katika rangi mbili za kuvutia, Titanium Grey na Mountain Shade. Wateja watakaonunua simu hii kwenye maduka ya Airtel pia watafurahia vifurushi vya kipekee vya Airtel na ofa zilizoundwa ili kuongeza uwezo wa simu.
Ushirikiano huu wa kimkakati ni ishara tosha ya maono ya pamoja kati ya Airtel na Infinix, kuwawezesha Watanzania kwa teknolojia inayorahisisha, kuinua na kutajirisha maisha ya kila siku.