Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
SERIKALI Imesaini mikataba minne kwa ajili ya kununua asilimia 20 ya dhahabu inayochimbwa na kusafishwa hapa nchi,ambayo itanunuliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT),ili kuhakikisha wanakuza uchumi WA nchi na wachimbaji kwa ujumla.
Utiaji saini huo ni moja ya utekelezaji wa kifungu cha sheria ya Madini ambacho kinawataka wachimbaji kufanya hivyo,ili madini yaweze kubakia nchini.
Makampuni yaliyosaini Mikataba hiyo ilioshuhudiwa na Waziri wa Fedha,waziri wa Madini pamoja na Gavana wa Benki Kuu (BOT),ni Geita Gold Mine,(GGM), Shanta Mining,Bakrifu na Kiwanda cha usafishaji wa Dhahabu
Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Mwigulu Nchemba katika hafla ya ya utiaji saini wa mikataba ya Ununuzi na Usafishaji wa Dhahabu kati ya Benki Kuu ya Tanzania na Makampuni ya Madini na Kiwanda cha usafishaji Dhahabu hapa nchini.
Dkt Nchemba amesema hatua hiyo ni muhimu sana kwa sababu itazidi kuchochea ukuaji wa uchumi hapa nchini lakini pia itazidi kuwainua wachimbaji wakunwa na wadogo wa madini hapa nchini.
Aidha Dkt Nchemba amesema mkakati huo uwe endelevu kutokana na kwamba utasaidia kuongeza fedha za kigeni pamoja na kuo geza kukuza uchumi wa nchi lakini kuwa na akiba ya dhahabu nchini.
Waziri Dkt Nchemba ametoa wito Kwa viwanda vya kisafisha dhahabu hapa nchini kuhakikisha wanaongeza uwezo wa kusafisha madini hayo ili waweze kufikia viwango vya kupata ithibati ya kimataifa.
Alimpongeza waziri wa Madini Antony Mavunde kutokana na kazi kubwa anayofanya pamoja na Gavana wa BOT Emmanuel Tutuba iliopelekea kufikia hatua hii ya kusaini mikataba hiyo.
Waziri DKt Nchemba aliwataka BOT kuendelea na mikakati yao ili kuhakikisha ifikapo 2026 wanafikia lengo la kununua dhahabu tani sita kutoka kwa wachimbaji madini hapa nchini.
Naye Gavana wa BOT Emmanuel Tutuba aliishkuru serikali kutokana na ushirikiano inayowapa hadi kufikia kusaini mikataba hiyo pamoja na makampuni hayo hapa nchini.
Tutuba amesema hadi kufikia Juni 13 2025 BOT imenunua jumla ya kilo za dhahabu safi 5022 ambazo ni sawa na tani 5.022 jambo ambalo ni ongezeko kubwa kwa serikali huku akisisitiza wataendelea kununua dhahabu hizo.
Mbali na hayo Tutuba alisisitiza BOT itaendelea kutoa malipo yao kwa wakati ambayo ni ndani ya masaa 24 wahusika wanapata malipo yao.
Waziri wa Madini Antony Mavunde amesema kutokana na ununuzi wa dhahabu unaofanywa na BOT Tanzania inakwenda kuingia kwenye 10 ya nchi ambayo ina akiba ya dhahabu huku akisema wizara ya Madini inakwenda kuvuka lengo la kuingiza sh trioni moja katika mfuko mkuu WA serikali.
Naye Naibu Mwaansheria Mkuu wa Serikali Samwel Maneno amesema mkakati huu ni muhimu sana kwa sababu unaisaidia serikali kuwa na akiba ya fedha za kigeni.