MJUMBE wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) ya CCM, Ramadhan Mlao, amewataka vijana kujitokeza kuommba ridhaa ya kugombea nafasi mbalimbaliza uongozi katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Amesema vijana hawatakiwi kuwa ‘wabena mabegi’ ya wagombea badala yake washiriki kikamilifu katika uchaguzi huo kuwani nafasi za uongozi.
Mlao,aliyasema hayo, Dar es Salaam, alipofungua mafunzo maalumu yaliyoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Ilala.
“Tunaanza uchaghuzi wa ndani kabla ya kufanya uchaguzi wa nje. Uchaguzi wa ndani kila mwanachama wa CCM anayo haki ya kuchukua fomu na kuomba ridhaa kugombea,”amesema Mlao.
Amewaomba vijana wenye nia na dhamira ya kuomba nafasi kujitokeze kuomba nafasi hizo.
“Chama hiki kiliasisiwa na Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume wakiwa vijana wachanga kabisa.Walipabana kwa dhati wakakijenga. Vijana hatuna namna ya kukaa kando na nafasi hizi zinazo tangazwa,”alieleza.
Amesema, haipendezi vijana kusalia kuwa wapambe wa wagombea na kuwabebea mabegi watia nia.
Aidha aliitaka UVCCM kuwa makini na wana chama watakao jitokeza kuomba ridhaa ya kuombea.
“Watakao chukua fomu kuomba ridhaa ni watu tunaoshi nao katika mitaa yetu.Tunajua tabia zao, mienendo yao na hurka zao. Tusikubali kuingia katika mtego kuchagua mtu ambaye tunapenbdezwa naye sisi tu ikiwa jamii haipendezwi naye,”ameeleza Mlao.
Amebainisha, kura katika uchaguzi wanje hazitapigwa na wana CCM tu bali hata wasio wanachama wa CCM, hivyo ni muhimu kusimamisha mgombea ambaye atakubalika na wote.
“Pia tusisimamishe wagombea ambao tutapata kazi kubwa ya kuwapamba na kuwa nadi.CCM inauzika . Tusipeleke wagombea wasio uzika wakakipa taabu Chama katika kuwa nad,”amesema.
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Ilala, Juma Mizingu, alieleza, lengo la mafunzo hayo ni kuwandaa vijana kuelekea uchaguzi mkuu.
“Ifikapo Oktoba mwaka huu vijana tunahakikisha Rais Dk. Samia, anapata kura za kishindo. Tunaendelea kujipanga kuhakikisha pia CCM inapata ushindi katika kata zote 36 za Wilaya ya Ilala na majimbo yote matatu,”amesema Mizungu.
Amesema, UVVCM Wilaya ya Ilala inampongeza Rais Dk. Samia, kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo wilayani humo ambao ni utekelezaji wa Ilani ya CCM.
“Tumeshuhudia Rais Dk. Samia, akielekeza fedha nyingi katika miradi ya maendeleo. Tunamhakikishia vijana Wilaya ya Ilala tutampa kura za kishindo na tuko tayari kupambania ushindi huu,”ameeleza.