OR-TAMISEMI
Mkoa wa Mwanza umeibuka mshindi wa jumla katika mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Tanzania kwa Shule za Msingi ambayo imehitimishwa leo juni 18,2025 Mkoani Iringa.
Mwanza imeshika nafasi ya kwanza baada ya kufanya vizuri katika michezo mbalimbali iliyochezwa kwenye mashindano ya mwaka huu ambayo yalihusisha michezo ya Cricket,Goal ball na Netiboli (Wasichana na Wavulana).
Michezo mingine ni Riadha, Soka wasichana na wavulana, Netiboli, mipra wa mikono, Wavu,Kikapu,soka maalumu na Sanaa za Maonesho uliojumuisha Ngoma za Asili, Kwaya na Muziki wa kizazi kipya.
Mashindano ya UMITASHUMTA & UMISSETA 2025 yalifunguliwa rasmi juni 9,2025 na Waziri Mkuu Mh.Kassim Majaliwa na yamehitimishwa juni 18,2025 na Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Omary Kipanga.
UMITASHUMTA ya mwaka huu pia ilitumika kutoa hamasa ya kushiri kuchaguzi mkuu, na kauli mbiu ilikuwa “Viongozi bora ni msingi wa maendeleo na Taaluma, Sanaa na Michezo, Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa Amani na Utulivi.
Ofisi ya Rais-TAMISEMI ndiyo iliyoandaa na kuratibu mashindano hayo, ikishirikiana Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.