Na John Bukuku, Morogoro
WAANDISHI wa habari za mitandaoni wanaoandika habari za Wizara ya Fedha wamejengewa uwezo kuhusu Usimamizi wa Mnyororo wa Ugavi katika semina inayofanyika leo mjini Morogoro.
Akifungua semina hiyo Dkt. Frederick Mwakibinga Kamishna Idara ya Sera za Ununuzi Wizara ya Fedha amesema kuwa, lengo la semina hiyo ni kulenga na kutoa uelewa kuhusu usimamizi wa mnyororo wa ugavi .
Amesema kuwa ,kupitia taarifa tunazozipata kwa wananchi lakini pia tutazidi kujenga taswira nzuri ya nchi yetu katika jumuiya ya kimataifa .
Amesema kuwa, mnyororo huo pamoja na kwamba umekuwa ukitumika vizuri zaidi katika sekta za kibiashara kwa maana ya sekta binafsi lakini unakuwa na manufaa pia .
“Kupitia kwenu ningependa kuwafikia wananchi wa Tanzania waweze kuufahamu vizuri umuhimu wa huo mnyororo na hivyo kuweza kujipanga na kuusimamia vizuri ili uwe na matokeo yanayotarajiwa .”
“Nimefarijika pia kwa kuona mwitikio mkubwa wa nyie kushiriki katika mafunzo haya mwitikio huu unaonyesha dhamira ya pamoja ya kuendeleza ushirikiano kati ya wizara ya fedha na nyie wanahabari .”amesema .
Amesema kuwa, mafunzo hayo muhimu yatawajengea uelewa ambao utatumika katika kuwahabarisha watanzania pamoja na wote mnaoweza kuwafikia .
“Kama mnavyofahamu nyie ndio sauti na sauti unaweza kuitumia vyovyote unavyotaka unaweza kutumia kujenga au kubomoa .”amesema .
Ameongeza kuwa, serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi sana katika kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma bora na kamilifu kwa mfano zaidi ya asilimia 70 ya bajeti ya serikali hutumika katika kununua vifaa ,huduma ambao vyote vinalenga katika kwenda kuwahudumia wananchi wa Tanzania .
Amefafanua kuwa ,fedha hizi ambazo zinanunua vitu huduma na mambo mengine kwa ajili ya kuwahudumia wananchi ile huduma itapatikana kupitia mnyororo wa ugavi toka pesa inatoka ,mahitaji ya ununuzi yanatengenezwa vinavyonunuliwa ,kupokelewa vinasambazwa hadi kumfikia mtu wa mwisho .
“Hizo hatua zote ndizo zinatengeneza mnyororo na hivyo vitu vinatakiwa viwe na muunganiko ambao utatengeneza flow ambayo itakuwa na manufaa.”amesema .
Amefafanua kuwa ,muunganiko huo hautakuwa umekaa vizuri ukaea una matundumatundu huko njiani na fedha zikaanza kufuja huko njiani na mwisho wa siku kitakachofika kule hakitakuwa timilifu na hilo sio lengo letu.
Amesema kuwa ,lengo letu ni kuhakikisha kuwa thamani ya fedha ifike kule mwisho na ikifika kule mwisho kutakuwa na matokeo makubwa sana na yataonekana hata kwa macho .
“Ni vizuri sana tutambue athari zinazotokana na kutokuwepo kwa usimamizi thabiti wa shughuli zilizopo katika mnyororo wa ugavi kwani ni jambo la msingi kwa maendeleo ya Taifa kwa kuzitambua athari hizo tunaweza kujiweka katika mazingira mazuri ya kuweza kutengeneza miongozo na mikakati mbalimbali ya utekelezaji ili kuimarisha usimamizi na hata kuepukana na athari hizo.”amesema .
“Kumjua adui ni sehemu ya ushindi na ndio maana mnapopambana kwenye mashindano yoyote yale hata ya kawaida lazima muwe na siri zenu za ushindi ambazo mmeziweka ukigawa siri zako zote washindani wako wakakujua ulivyo watakumaliza kirahisi kwani wanajua nguvu yako ilipo na udhaifu wako ulipo .”amesema .
Amewasihi kulitumia jukwaa hilo kama fursa muhimu ya kujifunza kujadili,na kubadilishana uzoefu na hata kushauri juu ya maswala ya usimamizi wa shughuli za mnyororo wa ugavi kwani kwa kufanya hivyo watajiweka kwenye nafasi nzuri sana ya kuhabarisha umma wa Tanzania kwa usahihi kupitia vyombo vya habari .