Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali za Maji, Robert Sunday,akikata utepe kuashiria uzinduzi na kukabidhi kisima cha Maji katika eneo la Shule ya Msingi ya Buigiri wasioona Wilayani Chamwino mkoani Dodoma kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji,hafla iliyofanyika leo Juni 18,2025.
Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali za Maji, Robert Sunday,akizungumza na waananchi mara baada ya kuzindua na kukabidhi kisima cha Maji katika eneo la Shule ya Msingi ya Buigiri wasioona Wilayani Chamwino mkoani Dodoma kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji,hafla iliyofanyika leo Juni 18,2025.
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali za Maji, Robert Sunday,(hayupo pichani) mara baada ya kuzindua na kukabidhi kisima cha Maji katika eneo la Shule ya Msingi ya Buigiri wasioona Wilayani Chamwino mkoani Dodoma kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji,hafla iliyofanyika leo Juni 18,2025.
…
WIZARA ya Maji imezindua na kukabidhi kisima cha Maji chenye uwezo wa kuzalisha lita 12000 kwa siku ambacho kitahudumia watu 120 wanaoishi katika eneo la Shule ya Msingi ya Buigiri wasioona wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, mara baada ya kukabidhi mradi huo,Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali za Maji, Robert Sunday, amesema mradi huo umefadhiliwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC) kwa kupata fedha kutoka Benki ya Dunia(WB).
Amesema uchimbaji wa kisima hicho ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji chini ya ardhi unaotekelezwa na Taasisi inayosimamia rasilimali za maji chini ya ardhi katika Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC-GMI) katika nchi 16 za SADC.
Amesema hapa nchini mradi huu umetekelezwa katika kata ya Nzuguni na Buigiri jijini Dodoma na kwamba lengo la kuutekeleza ni kuendeleza juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha makao makuu ya nchi yanapata maji safi na salama yenye kujitosheleza.
“Ameishukuru SADC GMI na WB na wadau wote waliowezesha itekelezaji wa mradi huo ambao utakuwa na manufaa makubwa huku akisisitiza kuwa Wizara itaendelea kugusa maisha ya watu na kutimiza lengo la upatikanaji wa huduma bora ikiwemo maji safi na salama kwa ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla,”amesema
Kwa upande wake Mwakilishi wa Benki ya Dunia (WB), Palesa Mokorosi amesema kuwa wamekuwa wakiisaidia SADC-GMI tangu mwaka 2014 ambapo awamu ya kwanza mradi huo ulitekelezwa Dar es Salaam Kimbiji na awamu ya pili Dodoma.
Naye Mkurugenzi wa SADC -GMI, Mhandisi James Sauramba amesema kuwa wametekeleza miradi ya aina hiyo zaidi ya 24 katika nchi 16 wanachama za SADC huku akitoa wito utunzwe ili uzae matunda tarajiwa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule, Joel Mwaka ameishukuru serikali kwa mradi huo wa kisima ambao kwa kiasi kikubwa utatatua changamoto ya upatikanaji huduma ya maji katika eneo hilo.
