Mwenyekiti wa Ccm Mkoa wa Iringa Daud Yassin akikabidhi fedha milioni 10 kwa Chifu wa Wahehe Adam .Mkwawa fedha zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya Hehe Day.
……….
NA DENIS MLOWE IRINGA
MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Iringa, Daudi Yasin, amemkabidhi Chief Adam Mkwawa kiasi cha shilingi milioni 10, mchango maalum kutoka kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa ajili ya kuunga mkono maadhimisho ya Hehe Day.
Makabidhiano hayo yamefanyika kwa heshima kubwa katika mazingira ya kuenzi historia ya jamii ya Wahehe, na kuthibitisha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuhifadhi, kukuza na kutangaza urithi wa utamaduni wa Kitanzania.
Katika hotuba yake, Ndugu Daudi Yasin amesisitiza kuwa mchango huu ni ishara ya kuthamini mchango wa familia ya Mkwawa na jamii ya Wahehe katika historia ya ukombozi wa taifa, pamoja na kuimarisha mshikamano wa kitaifa kupitia utamaduni.
Hehe Day ni siku muhimu ya kutafakari historia, kuenzi mashujaa wa jadi, na kuimarisha urithi wa jamii ya Wahehe kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Watu mbalimbali wamehudhulia siku hiyo iliyofanyika leo katika viwanja vya Kalenga.