MKurugenzi Mtendaji wa Makumbusho ya Chifu Ndaskoi, Ol-aiguenani Meshack Ndaskoi akizungumza katika zoezi hilo.la kufanya usafi katika mto huo.



Baadhi ya wananchi wakiendelea na zoezi la kufanya usafi kwenye chanzo cha mto huo jijini Arusha
Happy Lazaro,Arusha .
Wananchi wa Kata za Moshono na Ol-oirien wamejitokeza kwa wingi kuondoa takataka za plastiti katika Mto wa Enchoro e ndia na kingo zake ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Mazingira duniani ambayo Kauli mbiu ya mwaka huu wa 2025 ni “Pinga Uchafuzi wa Plastiki” .
Chanzo cha Mto huu unaanzia eneo la Machaare na unatumika kama mpaka kati ya Kata hizi ambapo upo upande wa Mashariki mwa Ol-oirien na Magharibi mwa Moshono.
Shughuli hiyo ya kusafisha mazingira na kuweka katika hali safi na salama, imeandaliwa na Ola-iguenani Meshack Ndaskoi, Mkurugenzi wa Mtendaji wa Makumbusho ya Kumbukumbu ya Chifu Ndaskoi iliyopo Moshono katika Jiji la Arusha.
Makumbusho hii pamoja na kujishughulisha na masuala ya Kimakumbusho pia inajishughulisha utunzaji wa miti na mimea ya sili mbayo iko katika hatari ya kupotea na kuhifadhi na kutunza mazingira.
Wakizungumza wakati wa kufanya usafi kwenye mto huo, wananchi hao wamesema kuwa wamefikia uwamzi wa kuitikia wito wa kufanya usafi kwenye mto huo kwa lengo la kutunza mazingira na kuhakikisha yanabaki salama muda wote kwani kuna uchafuzi mkubwa unaofanywa na baadhi ya wananchi kwa kutupa taka zao kwenye mto huo na katika maeneo yao ambapo wakati wa mvua maji yanapeleka mtoni na zingine kunasa kwenye kingo za mto.
Zakaria Kipuyo, mmoja wa wananchi walioshirki zoezi hilo amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuhamasisha jamii kutunza na kuhifadhi vyanzo vya maji kwani wengi wao hivi sasa wamejisahau badala ya kuhifadhi taka na kwenda kutupa sehemu husika wanatupa ovyo.
Tunampongeaza na kumshukuru sana Mkurugenzi Mtendaji wa Makumbusho hii kwa kutuhamasisha kufanya usafi kwenye mto huu jambo ambalo linaleta tija kubwa kwani ni muhimu sana tukayatunza na kuhifadhi mto huu kwa kuwa kuna baadhi ya watu wanaoyatumia maji kutoka mto huu kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwamo kunywa na kupikia. “amesema” .
Naye mwananchi mwingine Jonas Ndaskoi, amesema kuwa jamii inatakiwa kuhamasihshwa sana kuona umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji kwani bado mwammko wa jamii katika kutunza mazingira ni mdogo sana jambo linalosababisha mazingira kuendelea kuchafuliwa.
Kwa upande wake MKurugenzi Mtendaji wa Makumbusho ya Chifu Ndaskoi, Ol-aiguenani Meshack Ndaskoi amesema kuwa Makumbusho hiyo imejikita kutunza historia ya Arusha pamoja na mila na desturi ya wenyeji hususan Wamaasai pamoja na Wameru.
Pia Mkumbusho hiyo ina bustani inayotunza miti na mimea ya asili ambayo iko katika hatari ya kupotea na kuhifadhi mazingira.
Ndaskoi amefafanua kwamba katika pembeni mwa Bustani hiyo kuna mto ambao unatiririsha maji yake mwaka mzima ambapo baadhi ya watu wanatumia maji yake kunywa, kupikia, kumwagilia bustani lakini kwa bahati mbaya kumekuwepo na uchafuzi mkubwa wa mazingira ya mto huo kwa baadhi ya wananchi hutupa uchafu wa kila aina ndani ya mto, jambo ambalo linachangia uchafu wa mazingira na maji haya kutokuwa masafi na salama mbalimbali.
Kutokana na changamoto hiyo, taasisi yetu imeona kwamba kuna haja ya kuhamasisha jamii kama sehemu ya majukumu yake ili kushiriki katika kutunza mazingira kwa kuondoa uchafu kwenye mto huo ili yawe masafi na kunusuru viumbe kwenye maji na afya za binadamu na mifugo.
Ameongeza kuwa , tangu Makumbusho hiyo kuanzishwa mwaka 2020 hadi sasa kila mwaka wamakuwa wakihamasisha jamii hususan wanaoishi maeneo ya jirani na mto huo kuuungana pamoja katika kufanya usafi hususan baada ya mvua za masika kukatika au kupungua. Wamekuwa wakitoa takataka nyingi ya aina mbalimbali kwenye maji ikiwemo plastiki, vifungashio, nguo zilizonasa kwenye miti kando kando ya mto.
“Nafarijika na ninafurahi kuona kwamba jitihada hizi zimezaa matunda chanya kuwa kuwa uelewa miongoni mwa wanajamii wanaoishi maeneo haya unazidi kuongeza juu ya kuhifadhi na kutunza mazingira.”amesema .
Ndaskoi amesema lengo kuu ni kuhamasisha jamii ili wote tutambue umuhimu wa kuhifadhi mazingira kwani yakiharibiwa na mtu mmoja inasababisha madhara kwa wengi.
Aidha, ametoa wito kwa jamii kuchukua hatua mbalimbali na kupunguza uharibifu wa mazingira kwa kutotupa taka hovyo au kuchoma hawa plastiki kutokana na madhara makubwa kwa binadamu na mifugo,vilevile kutumia baadhi ya vifaa vya kubebea vitu zaidi ya mara moja.
“Tunashukuru kwamba Serikali yetu kwa kupitia Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa kuweka utaratibu mzuri wa kukusanya na kusomba takataka kwa kuweka vituo katika maeneo mbalimbali katika mitaa. “amesema .
Hata hivyo bado kuna watu wachache ambao hawatumii huduma hii badala yake wanatupa ovyo takataka zao matokeo yake kuwaadhriri wengi. Hivyo kuna Serikali pamoja na wadau wengine kuendelea kufanya jitihada za makusudi na endelevu ya kuhakikisha kuwa jamii yote inatambua umuhimu wa kutunza na kuhifadhi mazingira kama njia ya kumaliza tatizo hili .