Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC Bw.Salvator Chuwa ,akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 20,2025 jijini Dodoma kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Udhibiti wa Bidhaa Bandia Duniani yanayotarajia kufanyika Juni 25,mwaka huu jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
TUME ya Ushindani (FCC) imesema biashara ya bidhaa bandia ni tishio kwa usalama wa soko la ndani na nafasi ya Tanzania katika soko la pamoja la Afrika, huku ikibainisha kuwa bidhaa hizo sasa zinachangia hadi asilimia 3.3 ya biashara ya kimataifa.
Hayo yameelezwa leo Juni 20,2025 na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC Bw.Salvator Chuwa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Udhibiti wa Bidhaa Bandia Duniani,ambapo amesema kuwa biashara ya bidhaa bandia huondoa ushindani wa haki, hupunguza mapato ya Serikali, na huharibu mazingira ya uwekezaji.
“Bidhaa hizo si tu zinakiuka sheria za ndani, bali pia zinavunja mikataba ya kimataifa kama ile ya Shirika la Biashara Ulimwenguni (WTO), hivyo kuhatarisha nafasi ya Tanzania katika ushiriki wa biashara ya kimataifa na ya kikanda.”amesema Bw.Chuwa
Katika kukabiliana na hali hiyo, FCC imeimarisha usimamizi kwa kufungua ofisi za kikanda katika mikoa ya Mwanza, Arusha na Mbeya ili kudhibiti uingizwaji wa bidhaa bandia kupitia mipaka mikuu kama Tunduma, Namanga na Kasumulu.
Aidha Bw.Chuwa amesema FCC imekuwa ikitoa elimu kwa walaji, wafanyabiashara, wakuu wa mikoa, wabunge, vyombo vya habari, wanavyuo na taasisi za kimataifa kuhusu madhara ya bidhaa bandia na wajibu wa kila mmoja katika kukabiliana nazo.
Maadhimisho ya mwaka huu yanafanyika jijini Dodoma yakibeba kaulimbiu “Kujenga Kesho Salama, Kutetea Uhalisia kwa Uongozi Thabiti”, yakihusisha vipindi vya redio, runinga na mitandao ya kijamii, yakilenga kuongeza uelewa wa jamii kuhusu uhalisia wa bidhaa.
Kilele cha maadhimisho hayo kitafanyika Juni 25, 2025 katika Ukumbi wa Mabeo jijini Dodoma na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo
FCC imetoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya bidhaa bandia kwa kutoa taarifa sahihi, huku waandishi wa habari wakihimizwa kuwa mabalozi wa elimu kwa jamii.