Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha, Bi. Janeth Hiza, akipata maelezo kwa Afisa Mwandamizi wa Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Bw. George Kilo, kuhusu elimu ya usimamizi wa mali za Serikali unavyotolewa katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.
Na. Peter Haule na Saidina Msangi, Dodoma
Wananchi wenye Simu janja wametakiwa kupakua Aplikesheni ya Mfumo wa Kielektroniki wa Malipo ya Serikali (GePG) ili kuwarahisishia katika ufanyaji wa malipo mbalimbali ya huduma za Serikali.
Hayo yameelezwa na Afisa Mwandamizi wa Idara ya Usimamizi wa Mifumo ya Fedha na Tehama Wizara ya Fedha, Bw. Charles Maganga, wakati akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.
Bw. Maganga alisema kuwa Aplikesheni ya GePG Tanzania ni programu ya simu ambayo inawezesha watumiaji kuuliza, kutathmini na kulipia ankala za Serikali kwa kupitia Simu janja ya Kiganjani (Smartphone).
Alisema Aplikesheni hiyo inarahisisha ulipaji kwa uharaka zaidi na utunzaji wa Kumbukumbu za malipo ambapo mtumiaji pia anaweza kupata taarifa za ankala (Biliş) kuhakiki mita namba, kununua Luku, kuandaa na kulipia Loss Report pamoja na kukadiria kodi ya ardhi.
Pia inaweza kutumika kulipia maegesho, kulipa faini za makosa ya barabarani na kupata ankara ya maji kwa kutumia akaunti namba na huduma nyingine za Serikali,
inamsaidia mtumiaji kuhakiki namba ya malipo, Risiti ya Benki na Risiti ya GePG.

Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha, Bi. Janeth Hiza, akipata maelezo kwa Afisa Mwandamizi wa Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Bw. George Kilo, kuhusu elimu ya usimamizi wa mali za Serikali unavyotolewa katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.


Afisa Mwandamizi wa Idara ya Usimamizi wa Mifumo ya Fedha na Tehama, Bw. Charles Maganga, akigawa kipeperushi kwa mtoto Leandra Mayenga, kinachohusu maelekezo ya matumizi ya Aplikesheni ya Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.

Afisa Mwandamizi wa Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Bw. George Kilo, akitoa elimu ya usimamizi wa mali za Serikali kwa mkazi wa Dodoma, Bw. Enock Babu, wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.

Afisa Mwandamizi wa Kitengo cha Huduma za Mfuko Mkuu wa Serikali Wizara ya Fedha, CPA Farida Manilwa, akitoa elimu kwa Bi Weraisaria Mushi kuhusu huduma zinazotolewa na Mfuko huo, wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.

Afisa Mkuu wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Bw. Salim Kimaro, akitoa elimu ya fedha kuhusu akiba, uwekezaji na matumizi kwa wakazi wa Dodoma waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha, Wiki ya Utumishi wa Umma, viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.

Mtumishi wa Hazina Saccos, Bi. Violeth Mdemu, akitoa elimu kwa Bw. Gasper Mwakalinga, kuhusu hatua za kujiunga na Saccos hiyo na faida zake kwa watumishi wa umma alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.

Afisa Hesabu wa Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali Wizara ya Fedha, Bi. Mercelina Haule akitoa elimu kuhusu masuala ya kihasibu kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.

Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha, Bi. Janeth Hiza, akitoa maelekezo kwa Maafisa wa Wizara ya Fedha wanaotoa huduma kwa wananchi kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma, kuzingatia weledi na nidhamu ili wanachi wanufaike na maadhimisho hayo.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)