Na. Peter Haule na Saidina Msangi, Dodoma
Wananchi wenye Simu janja wametakiwa kupakua Aplikesheni ya Mfumo wa Kielektroniki wa Malipo ya Serikali (GePG) ili kuwarahisishia katika ufanyaji wa malipo mbalimbali ya huduma za Serikali.
Hayo yameelezwa na Afisa Mwandamizi wa Idara ya Usimamizi wa Mifumo ya Fedha na Tehama Wizara ya Fedha, Bw. Charles Maganga, wakati akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.
Bw. Maganga alisema kuwa Aplikesheni ya GePG Tanzania ni programu ya simu ambayo inawezesha watumiaji kuuliza, kutathmini na kulipia ankala za Serikali kwa kupitia Simu janja ya Kiganjani (Smartphone).
Alisema Aplikesheni hiyo inarahisisha ulipaji kwa uharaka zaidi na utunzaji wa Kumbukumbu za malipo ambapo mtumiaji pia anaweza kupata taarifa za ankala (Biliş) kuhakiki mita namba, kununua Luku, kuandaa na kulipia Loss Report pamoja na kukadiria kodi ya ardhi.
Pia inaweza kutumika kulipia maegesho, kulipa faini za makosa ya barabarani na kupata ankara ya maji kwa kutumia akaunti namba na huduma nyingine za Serikali,
inamsaidia mtumiaji kuhakiki namba ya malipo, Risiti ya Benki na Risiti ya GePG.








(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)