……….
Kampuni ya uzalishaji na ufungaji wa vifaa vya umeme Jua Compact Energies inayoshiriki katika maonesho makubwa ya Utalii na Uwekezeji visiwani Zanzibat maarufu kama ‘Zanzibar Tourism & Investment Show 2025) imesema ipo tayari kusaidia ukuaji wa sekta ya uchumi wa buluuu visiwani humo kwa kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya nishati jua katika kusaidia ukuaji uchumi.
Akiongea wakati wa maonesho hayo , Meneja Masoko na Mauzo wa kampuni hiyo yenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam Fred Pantaleo Msafiri amesema kuwa uchumi wa Zanzibar chini ya Rais Hussen Ali Mwinyi unakuwa kwa kasi kwa maendeleo yanayofanywa na Serikali na wawekezaji, hivyo wana kila sababu ya kusaidia jitihada hizo.
“Maendeleo ya nishati mbadala yanakuwa kwa kasi sana duniani kwa sababu ya upatikanaji wake kuwa rahisi na uhakika,”
“Kwa uzoefu wetu tuliokuwa nao katika uzalishaji na ufungaji wa vifaa vya umeme, tumeona haja ya kushiriki maonesho haya na kuja kuonesha teknolojia ambayo inaweza kusaidia katika sekta mbalimbali kuanzia nyumbani, viwandani na maofisi,” amesema Pantaleo.
Amesema kuwa maeneo mengi ya utekelezaji wa uchumi wa buluu na wa kawaida unahitaji nishati safi na salama , hivyo wakati umefika kwa Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla kutumia rasilimali umeme jua na vinafaa vinavyotumia nishati hiyo ambayo haihitaji malipo ya kila wakati.
Hivi karibuni, Compact pia ilishiriki katika maonesho maarufu ya Arusha Kili Fair na kuwasilisha miradi yake ya mafanikio katika sekta ya utalii, ikijumuisha mifumo ya umeme isiyotegemea gridi (off-grid) na mifumo ya mseto (hybrid) iliyosimikwa kwenye malazi ya watalii kama vile lodji, kambi za mahema, mapumziko ya kiikolojia (eco-resorts), na maeneo ya mbali ya kitalii kote Tanzania.
Ufungaji huu umechangia kupunguza utegemezi wa nishati ya mafuta, kupunguza utoaji wa hewa ukaa, na kuboresha upatikanaji wa nishati—vipengele muhimu katika uendeshaji endelevu wa huduma za malazi.
Wananchi wanaoshiriki maonesho ya Zanzibar pia walitembelea banda la kampuni hiyo Compact ili kufahamu zaidi kuhusu ubunifu wao katika teknolojia ya nishati ya jua—ikiwemo hita za maji za sola, hifadhi ya betri za lithiamu, na mifumo ya inverter ya mseto iliyoundwa kwa ajili ya magari ya safari katika sekta ya utalii.
Mmoja wa wananchi hao Juma Makame amesema kuwa mbali na kuisifu kampuni hiyo kwa uwekezaji ilioufanya, pia ametoa wito kwa jamii kutumia fursa ya utaalam wao katika kujiletea maendeleo ya haraka.
“Uzuri wa bidhaa zinazotokana na umeme jua hazina gharama , tofauti na nishati nyingine kama vile umeme au mafuta katika uzalishaji,”
“Lakini pia vitu vya nishati jua vinasaidia katika kutunza na kuhifadhi mazingira,” amesema,