Afisa mhifadhi mkuu wa hifadhi ya Serengeti ambaye ni kaimu mkuu wa idara ya utalii katika hifadhi hiyo akitoa taarifa ya hali ya hifadhi kwa waandishi wa habari waliotembelea hifadhi hiyo.
Picha zote na Musa Mwangoka
Mtalii Pranav Patel kutoka nchini Marekani akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzuri wa hifadhi ya Serengeti.
……………
Na
Neema Mtuka,Musoma
Mara: filamu ya maarufu ya Royal Tour aliyochezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu kwa lengo la kuhamasisha utalii nchini, imeanza kuleta neema ya ongezeko kubwa la watalii katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Afisa Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya Serengeti, Alex Choya ambaye ni kaimu mkuu wa idara ya Utalii katika hifadhi hiyo alisema hayo wakati akitoa taarifa ya hali ya uhifadhi kwa waandishi wa habari waliotembelea hifadhi hiyo.
Amesema tangu kuchezwa kwa filamu hiuo kumekuwa na mafuriko ya watalii wanaojitokeza kutembelea hifadhi hiyo na kujionea vivutio mbalimbali vilivyopo Serengeti.
Mhifadhi huyo, alisema tangu kuzinduliwa kwa filamu mei 7, 2022 visiwani Zanzibar na baadae nchini Marekani, hifadhi hiyo imetembelewa na 1334,054 kati yao 976,094 ni raia wa kigeni 357,960 ni watalii wa ndani.
Katika hatua nyingine, amesema mwitikio wa kutembelea hifadhi hiyo kwa viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini umekuwa mkubwa kwa siku za karibuni ambapo maaskofu na wachungaji 149 kutoka makanisa ya Waadventista Wasabato, Waislamu na viongozi wa dini za asili.
Mhifadhi huyo alisema inatia moyo kuona mwamko wa viongozi wa dini kutembelea hifadhi hiyo ni mkubwa,
Hivyo ni chachu kwa watanzania wengine kutembelea maeneo hayo na kujionea utajiri wa rasilimali zilizopo nchini ambazo wanapaswa kujivunia na kuzilinda kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Mmoja wa watalii kutoka nchini Marekani, jimbo la Califonia, Pranav Patel aliyeambatana na familia yake, alidai amevutia kutembelea hifadhi Serengeti ni kwa kuwa ni kati ya hifadhi chache bora duniani.
Mtalii huyo amesema umaarufu wa Hifadhi ya Serengeti ni sababu iliyomfanya yeye na familia yake kuja kujionia maajabu yaliyomo ndani ya hifadhi hiyo.
Hifadhi ya Serengeti ni tatu kwa ukubwa nchini, ikiwa na kilometa za mraba 14,763, ikitanguliwa na Mwalimu Nyerere, naya pili ni Ruaha.