Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mhandisi Anthony Sanga akizungumza kwenye mkutano huo jijini Arusha
………..
Happy Lazaro, Arusha
SERIKALI imefanikiwa kuandaa jumla ya mipango ya matumizi bora ya ardhi 2,480 katika kipindi cha miaka minne, ambapo vijiji 4,679 kati ya vijiji 12,333 vilivyopo nchini vimeingizwa kwenye mipango hiyo.
Akizungumza jijini Arusha kwa niaba ya Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratius Ndejembi, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mhandisi Anthony Sanga, amesema hatua hiyo inalenga kupunguza migogoro ya ardhi na kuhakikisha matumizi endelevu ya rasilimali ardhi nchini.
Mhandisi Sanga ameeleza kuwa tangu kupata uhuru, Serikali imekuwa ikiweka mikakati mbalimbali ya kupunguza migogoro ya ardhi, ikiwemo kuwahimiza wakurugenzi wa halmashauri kupima na kupanga matumizi bora ya ardhi angalau vijiji sita kila mwaka katika kila halmashauri nchini.
“Tumefikia hatua kubwa ya maendeleo kutokana na jitihada za Serikali, na ni jambo la kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza bajeti ya Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi. Kupitia fedha hizo, tumeweza kufanikisha upangaji wa vijiji 4,679 na bado vijiji 7,654 havijapangiwa,” amesema Sanga.
“Mipango ya matumizi bora ya ardhi hufanyika kuanzia ngazi ya vijiji kwa kushirikisha wananchi, jambo linalosaidia kupunguza migogoro ya ardhi ikiwemo ile ya mijini ambapo maeneo yamebanwa na watu wengi. Alishauri pia jamii za vijijini kuanza kujenga nyumba za ghorofa ili kuwezesha matumizi bora ya ardhi na kuacha nafasi kwa ajili ya kilimo na shughuli za maendeleo kama viwanda.”amesema .
Aidha, Mhandisi Sanga amesema wizara inaendelea kuhuisha ramani za msingi zilizowekwa tangu miaka ya 1970, sambamba na ununuzi wa ndege maalum na droni kwa ajili ya kurahisisha upimaji wa ardhi, utoaji wa hati za kimila, pamoja na kuboresha vituo vya upimaji kwa njia za kielektroniki.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya matumizi ya Ardhi Tanzania , Joseph Mafuru, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wadau wa sekta binafsi na Serikali katika kupanga maeneo ya vijiji na miji kwani mipango hiyo ni muhimu kwa maendeleo, hususan katika kutenga maeneo ya malisho na huduma za kijamii.
“Tumefanya kazi mwaka hu wa fedha unaenda kuisha julai tunaanza mwaka wa fedha mwingine kwa hiyo tunafanya assement ya wadau kwenye maswala ya upangaji wa matumizi ya ardhi .”amesema .
“Tunapokutana mwaka huu na wadau tunafanya assessment kwamba kwa mwaka mzima nini wamefanya na kwa mwaka unaokuja wa fedha kuanzia julai nini tunaenda kufanya hivyo sisi kama serikali ambao ndio msimamizi mkuu wa kazi hii tunawakaribisha wote wanakuja na tunawaambia tunakwenda wapi na malengo yetu kama serikali ambapo wao pia wanakuja kutuambia malengo yao na mipango kwenye hizo sekta .”amesema .
Amefafanua kuwa ,wanawapa mipango kuwa mwaka huu unaokuja wanaenda kuandaa mipango ya vijiji 4,000 wanaenda wilaya gani ili wao wajiandae na mipango yao ili isiwe inajirudia wanaangalia walichofanya changamoto zilikuwa zipi mafanikio yalikuwa vipi ili kupitia hiyo wajifunze ndio sababu kubwa ya kikao hicho .
Ameongeza kuwa, kwa mwaka huu wamepima vijiji mia sita hadi mia saba na wanapanga wanapima na kumilikisha kwenye vijiji mbalimbali .
“Kwa mwakani tuongeza spidi kubwa kwani tunakadiria kufanya vijiji 4,000 hivyo lazima tuwawaeleze watu tunakwenda wapi na wapi na wao watuambie plan zao .”amesema .
Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Raymond Mangwala, amesema wilaya yake inakumbwa na changamoto ya migogoro ya ardhi kutokana na umiliki wa ardhi kwa misingi ya kimila.ambapo kupitia mpango wa matumizi bora ya ardhi, vijiji 24 vimepimwa na kijiji kimoja tayari kimepata hati.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Remidius Mwema, amesema wilaya hiyo inaongoza kwa kuwa na migogoro ya ardhi kutokana na vijiji 63 kutokuwa na mipango bora ya matumizi ya ardhi. Alisisitiza viongozi wa vijiji, wilaya na mkoa kuheshimu mipaka iliyopo na kuepuka vitendo vya rushwa vinavyochochea migogoro.




