NA VICTOR MASANGU,BAGAMOYO
Mwenyekiti wa Jumuiya ya umoja wa wanawake (UWT) Wilaya ya Bagamoyo Mariam Mkalì amewaasa wanawake ķuhakikisha kwamba kuweka misingi mizuri ya kwenda kufanya kampeni za kistaarabu kwa kuzingatia kanuni na taratibu hasa katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa kikao cha Baraza la kawaida la jumuiya ambalo limefanyika katika Kata ya Msata na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa chama pamoja na jumuiya zake.
Mwenyekiti huyo amebainisha kwamba kwa sasa wanapaswa kuwa kitu kimoja na kushikamana kwa hali ya upendo na amani katika kipindi chote cha uchaguzi mkuu.
” Kikubwa ninachowaomba wanawake wenzangu tushikamane hasa katika kipindi chote cha uchaguzi na kwamba uchaguzi usiwe sababu za kutoleana lugha chafu,”amebainisha Mwenyekiti.
Kwa upande wake Katibu wa Jumuiya hiyo ya UWT Wilaya ya Bagamoyo Catherine Makungwa amewahimiza wanawake kunitokeza kwa wingi katika kumpa kura nyingi za kishindo Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan.
“Nawashukuru kwa dhati Wabunge, Mjumbe wa Baraza Kuu la UWT Taifa Mariam Ulega na Madiwani wote kwa michango yao mikubwa ambayo yameitoa katika kusaidia Jumuiya hiyo kufanikisha shughuli zao mbali mbali,”
“Pia namshukuru Mbunge wetu Muharami Mkenge, Ridhiwani, Hawa Mchafu, Dkt. Harris na Subira Mgalu ambao wamekuwa msaada mkubwa katika Jumuia yetu, wakiwemo wadau mbalimbali,” amesema Makungwa.
Kwa upande wao Madiwani wastaafu wa Viti Maalumu ambao wamemaliza muda wao wamesoma taarifa zao za Utekelezaji katika kipindi cha miaka mitano cha kuanzia mwaka 2020 hadi 2025.



