Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba(Mb) akiwasilisha bungeni Muswada wa Sheria ya fedha wa mwaka 2025, baada ya hapo jana Bunge kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali ya shilingi trilioni 56.49 kwa mwaka wa Fedha 2025/2026, jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) akimpongeza Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) baada ya kuwasilisha bungeni Muswada wa Sheria ya fedha wa mwaka 2025, baada ya hapo jana Bunge kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali ya shilingi trilioni 56.49 kwa mwaka wa Fedha 2025/2026, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba(Mb) na Naibu wake Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) wakifuatilia mijadala bungeni kuhusu Muswada wa Sheria ya fedha wa mwaka 2025, baada ya hapo jana Bunge kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali ya shilingi trilioni 56.49 kwa mwaka wa Fedha 2025/2026, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Naibu wake Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) wakiteta jambo bungeni kuhusu Muswada wa Sheria ya fedha wa mwaka 2025, baada ya hapo jana Bunge kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali ya shilingi trilioni 56.49 kwa mwaka wa Fedha 2025/2026, jijini Dodoma.

Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Natu El-maamry Mwamba (kulia) na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida, wakifuatilia uwasilishaji wa Muswada wa Sheria ya fedha wa mwaka 2025 bungeni, jijini Dodoma, baada ya hapo jana Bunge kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali ya shilingi trilioni 56.49 kwa mwaka wa Fedha 2025/2026. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha).
……….
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amewasilisha bungeni Muswada wa Sheria ya fedha wa mwaka 2025 baada ya hapo jana Bunge kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali ya shilingi trilioni 56.49 kwa mwaka wa Fedha 2025/2026.