Na Julius Okuly & Kadama Malunde – Morogoro
Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) umewataka waandishi wa habari kujihakikishia ulinzi na usalama wao binafsi kuelekea kipindi cha uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani unatakaofanyika  Mwezi Oktoba ,2025.
Kauli hiyo imetolewa Juni 25,2025 Mkoani Morogoro na Mjumbe wa Bodi ya UTPC na Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango na Fedha Bi. Lilian Lucas wakati akifungua mafunzo ya Wakufunzi kuhusu Usalama na Ulinzi (Safety and Security Training of Trainers – ToT) kwa viongozi wa Klabu za Waandishi wa Habari na waandishi wa habari walioteuliwa.
“Ulinzi na Usalama wa Mwandishi wa habari unaanza na yeye mwenyewe hivyo una jukumu la kujihakikishia usalama wako na ukizingatia tunaelekea katika uchaguzi mkuu ni kipindi ambacho Mwandishi  wa habari usipokuwa makini katika kazi zako unaweza kujikuta katika matatizo,” amesema Bi. Lilian.
Amesema mafunzo haya yanalenga kuwajengea uwezo waandishi waliochaguliwa kuwa wakufunzi wa wenzao kuhusu masuala ya usalama wa kimwili, kidijitali, na afya ya akili, hasa katika kipindi hiki ambapo mazingira ya kazi ya uandishi yameendelea kuwa hatarishi.
Bi. Lilian amewasisitiza waandishi kuwa makini na kujilinda wao wenyewe, hasa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu, akisema kuwa historia imeonyesha kuwa nyakati za uchaguzi waandishi huwa katika hatari kubwa ya kukumbwa na vitisho, ukatili au kukamatwa kiholela.
“Kuna wakati chaguzi zilipita na waandishi walifanyiwa vitendo vya unyanyasaji kutokana na ulinzi hafifu. Mafunzo haya yanapaswa kuwa chachu ya mabadiliko katika hilo,” ameongeza.
Bi. Lilian amesema  moja ya sababu zinazofanya Taasisi nyingi kukumbwa na changamoto ya upatikanaji wa fedha ni kutokana na kukosekana kwa matokeo yanayotarajiwa kwenye miradi.
 
“Tulikuwa tunatoa mafunzo kwa waandishi wengi sana, lakini wachache walifanya uandishi wenye tija kwa jamii. Hii imepelekea wafadhili kupoteza imani na hivyo kupunguza misaada yao,” amesema.
Naye Mratibu wa Mradi wa  Empowering Journalists for Informed Community Victor Maleko amesema wamepokea watu  197 ambao  walituma maombi ya kushiriki mafunzo hayo, lakini 36 pekee wameteuliwa, na kuwataka washiriki hao kutumia fursa waliyopewa kwa ubunifu na uzalendo mkubwa.
“Katika safari ya kuibadilisha UTPC kutoka nzuri hadi bora zaidi (‘From Good to Great’), tunahitaji mashujaa wachache wenye uwezo wa kufanya kazi kubwa. Nendeni mkathibitishe kuwa mlitakiwa kuwa hapa. Muwe chachu ya mabadiliko,” amewahimiza.
Aidha, amewataka washiriki kuthibitisha kwa vitendo thamani ya mafunzo hayo kupitia kazi zao na ushawishi kwa wenzao katika klabu.
“Sisi UTPC tunaamini kwamba mabadiliko ya kweli huletwa na watu wa kweli. Kuweni hadithi ya mabadiliko,” amesisitiza.
Amesema mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Empowering Journalists for Informed Community
(Kuwawezesha Waandishi wa Habari ili Jamii Iweze Kupata Taarifa Sahihi) ambao unafadhiliwa kwa Ushirikiano kati ya Umoja wa Ulaya (EU) na Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC).
Mradi unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya International Media Support (IMS), Union of Tanzania Press Clubs (UTPC), Media Council of Tanzania (MCT), JamiiAfrica, Nukta Africa na Tanzania Media Women’s Association (TAMWA).
Mafunzo hayo yanafanyika kuanzia tarehe 25 hadi 27 Juni 2025, ambapo waandishi wa habari wanaopewa mafunzo wanatarajiwa kutoa mafunzo hayo kwa waandishi wengine kupitia Press Clubs zao.
Mjumbe wa Bodi ya UTPC na Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango na Fedha Bi. Lilian Lucas akizungumza wakati akifungua mafunzo ya Wakufunzi kuhusu Usalama na Ulinzi (Safety and Security Training of Trainers – ToT) kwa viongozi wa Klabu za Waandishi wa Habari na waandishi wa habari

Mjumbe wa Bodi ya UTPC na Mwenyekiti wa kamati ya Mipango na Fedha Bi. Lilian Lucas akizungumza wakati akifungua mafunzo ya Wakufunzi kuhusu Usalama na Ulinzi (Safety and Security Training of Trainers – ToT) kwa viongozi wa Klabu za Waandishi wa Habari na waandishi wa habari
Mratibu wa Mradi wa Empowering Journalists for Informed Community Victor Maleko akizungumza wakati wa mafunzo ya Wakufunzi kuhusu Usalama na Ulinzi (Safety and Security Training of Trainers – ToT) kwa viongozi wa Klabu za Waandishi wa Habari na waandishi wa habari

Mratibu wa Mradi Empowering Journalists for Informed Community Victor Maleko akizungumza wakati wa mafunzo ya Wakufunzi kuhusu Usalama na Ulinzi (Safety and Security Training of Trainers – ToT) kwa viongozi wa Klabu za Waandishi wa Habari na waandishi wa habari
Mratibu wa Mradi wa Empowering Journalists for Informed Community Victor Maleko akizungumza wakati wa mafunzo ya Wakufunzi kuhusu Usalama na Ulinzi (Safety and Security Training of Trainers – ToT) kwa viongozi wa Klabu za Waandishi wa Habari na waandishi wa habari
Mratibu wa Mradi wa Empowering Journalists for Informed Community Victor Maleko akizungumza wakati wa mafunzo ya Wakufunzi kuhusu Usalama na Ulinzi (Safety and Security Training of Trainers – ToT) kwa viongozi wa Klabu za Waandishi wa Habari na waandishi wa habari

Mwezeshaji Lulu George akizungumza wakati wa mafunzo ya Wakufunzi kuhusu Usalama na Ulinzi (Safety and Security Training of Trainers – ToT) kwa viongozi wa Klabu za Waandishi wa Habari na waandishi wa habari