NA DENIS MLOWE IRINGA
KATIKA kuelekea mbio za kuwania uwakilishi wa wananchi mkoani Iringa , Mwanasheria na Mhadhiri Msaidizi wa Sheria Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mbeya, David Evance Komba ametangaza rasmi nia yake ya kugombea ubunge katika Jimbo la Isimani, Mkoa wa Iringa, kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Akizungumza na waandishi wa habari katika nyumbani kwake Iringa Mjini Komba mzaliwa wa kijiji cha Lwang’a kilichoko kata ya Kihorogota amesema uamuzi huo umetokana na msukumo mkubwa wa kuleta mabadiliko zaidi katika jimbo la Ismani ambalo lina hazina mbalimbali za uchocheo wa kiuchumi ikiwemo madini, kilimo cha mpungq , ufugaj na kilimo cha mazao mbalimbali.
Alisema kuwa Jimbo hili la Ismani kwa historia yake nzuri limekuwa likiongozwa n viongozi mbalimbali akiwemo Mzee wangu na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu na Bunge William Vengimem Lukuvi, ambao wamefanya kwa Jitihada zao kuleta maendeleo katika jimbo hili tangu Uhuru.
Aisema kuwa William Vengimemba Lukuvi historia itamkumbuka kama mbunge aliyekaa muda mrefu katika jimbo hili hivyo kutokumuelezea na kutothamini mchango wake itakuwa Si busara na wala haiakisi upinzani wa siasa safi za Chama cha mapinduzi ambacho Ilani na kauli mbiu yetu ya uchaguzi 2025/2030 inasema KAZI na UTU.
Alisisitiza kuwa CCM Imekuwa ikimuamini mzee wetu mh. William Vengimemba Lukuvi kwa awamu 6 kwa kupeperusha bendera ya Chama katika uchaguzi mkuu, na mara zote hizo amekipa ushindi wa kishindo chama chetu hivyo kuwa mwakilishi pekee wa jimbo la ismani kwa miaka 30 Na kwa moyo mkunjufu Nina mpongeza sana sana kwa uongozi wake
wenye mafanikio na kuleta mabadiliko chanya katika jimbo la Isman kwa kadri alivyoweza.
“Ameweza kusimamia serikali kujenge shule za kata katika kata zetu 13 ambazo mimi ni mnufaika wa juhudi hizi. Ameweza kusimamia uboreshaji wa miundombinu ya mawasiliano, huduma za afya na mengine mengi. Ni mtu mjinga pekee na asiye na shukrani ambaye anaweza kubeza mafanikio makubwa ambayo mzee Lukuvi ameyafanya katika kipindi cha miaka 30” Alisema
Komba alisema kuwa kuendeleza juhudi za Chama cha Mapinduzi ya kutumikia wananchi na kuleta mabadiliko kwa kasi ya Rais na MAMA yetu Dr. Samia Suluhu Hasan, basi ni wakati muafaka wa mimi kijana, mwenye maono makubwa na ya kisasa kupokea kijiti na kuanzia pale Alipoishia.
Alisema kuwq baada ya kusema hivyo ninawatangazia Rasmi wananchi wa Ismani kupitia kwenu waandishi wa habari, Nia yangu ya kugombea ubunge katika jimbo la isman kwa kufuata kwa Uadilifu michakato ya ndani ya chama.
Alimsifia William Vengimemba Lukuvi kuwa ni gwiji wa siasa za nchi hii na anafahamu miiko ya tamaduni 24 Chama chetu cha Mapinduzi. Anafahamu vema siasa za uongozi kuachiana Vijiti zilizoasisiwa na Hayati Julias Kambarage Nyerere.
Alivitaja vipaumbele vyake kwa wananchi kuwa suala zima la elimu , afya , kilimo ambapo katika kilimo endapo atateuliwa atahakikisha wanachimba mabwawa ya umwagiliaji Iengo likiwa ni kuwafanya walime nyakati zote na kuongeza uchumi wao na wa nchi.
Komba alisema kuwa Isman inahitaji kiongozi ambaye atawajali wananchi wote kwa kushinda jimboni ili kujua matatizo Ya wananchi na kinachoendelea katika jimbo, kusimamia miradi mikubwa ya serikali na kawapa wananchi mrejesho wa utekelezaji wa ilani na kuisemea serikali ya chama cha Mapinduzi.
Alimalizia kwa kumshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti CCM kwa kuendelea kutoa fursa vijana katika nafasi mbalimbali za kulitumika taifa na chama.
“Umeendelea kutuamini na kutuvumilia pale tunapoteleza. Umekuwa mlezi mkubwa kwa taifa kwa kutuvusha salama katika vipindi joto vya siasa za nchi hii, umeendelea kusimamia maendeleo ya nchi hivyo vijana hawakuda” Alisema.