Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Matumizi na Biashara ya Dawa za Kulevya Duniani yaliyofanyika kitaifa kwenye kituo cha mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Juni 26, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt, Felice Mafumiko (kushoto) alipotembelea mabanda ya maonesho katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Matumizi na Biashara ya Dawa za Kulevya Duniani yaliyofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Juni 26, 2025. Kushoto kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete na kulia kwake ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga. Wa tatu kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt Jim Yonazi na wa pili kushoto ni Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania, Aretas Lymo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya Washiriki wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Matumizi na Biashara ya Dawa za Kulevya Duniani yaliyofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Juni 26, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga akizungumza katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Matumizi na Biashara ya Dawa za Kulevya Duniani yaliyofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Juni 26, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kasssim Majaliwa akipokea kwa naiba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Tuzo maalum ya kutambua mchango wa Rais katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya alipomwakilisha Rais Samia katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Matumizi na Biashara ya Dawa za Kulevya Duniani yaliyofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Juni 26, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)