Kaimu mhifadhi mkuu wa hifadhi ya Saadani akizungumza kuhusu upekee wa hifadhi hiyo.
Picha na Musa Mwangoka
Mti aina ya mbuyu ambao upo ndani ya hifadhi ya taifa ya Saadani wenye taswira ya mama bikira maria.
……………..
Na Neema Mtuka ,Bagamoyo,
Pwani :Mbuyu wenye taswira ya Mama Bikira Maria, ni moja ya kivutio kinachofanya watalii wengi kutembelea hifadhi ya taifa ya Saadani iliyopo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Mwongozaji wa Watalii katika hifadhi hiyo, Fredy Neston, amewaeleza waandishi wa habari, wanaotembelea hifadhi hiyo na kujionea mbuyu huo ambao ni kivutio cha umefanya wageni wa ndani wenye imani ya dini ya kikristo kutembelea hifadhi hiyo.
Amesema mbuyu huo uliogundulika mwaka 2019 na mhifadhi mmoja aitwaye Tumaini Magesa ambapo wageni wengi hususani wakatoliki ufika eneo hilo na kusali huku wengine wakirejea kushukuru mara baada ya kufanikiwa mahitaji yao.
“Tuna vivutio vingi ndani ya hifadhi hii, lakini kwa miaka ya karibuni huu mti wa mbuyu ni kivutio kikubwa na kinavuta watu wengi na sio wakatoliki tu hata madhehebu mengine wanakuja kwa ajili ya kufanya ibada katika mti huo” amesisitiza.
Aidha, mmoja wa waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Lazaro Oliver Oliveria ambaye ni mzee wa Kanisa kutoka usharika wa Salei mkoani Arusha, amesema pamoja kuja kupumzika lakini kujifunza mambo imani kupitia Mbuyu huo wenye imani ya dini.
Amesema vitu vingine wamejifunza katika hifadhi hiyo ni pamoja ikiwamo kuona mambo ya kale, ambapo ni soko la watumwa, mbuyu ambao wakoloni waliutumia kunyonga watumwa waliodhofika kiafya.
Kwa upande wake, kaimu mhifadhi mkuu wa hifadhi ya Taifa ya Saadani, Daudi Goroni amesema upekee wa hifadhi hiyo ni pamoja na mto kukutana bahari na uwepo wa Sehemu pekee ya mazalia ya kasa ambayo huwezi kupata katika hifadhi yoyote ile.
Kwa upande wake, kaimu mhifadhi mkuu wa hifadhi ya Taifa ya Saadani, Daudi Gordon akizungumzia vivutio vilivyo ndani ya hifadhi hiyo.
Mti aina ya mbuyu ambao upo ndani ya hifadhi ya Taifa ya Saadani ambao una taswira ya Mama Bikira Maria Taswira hiyo uonekana vizuri ukiwa umbali wa mita 20.