Mbunge wa Jimbo la Solwa Mkoani Shinyanga Mhe. Ahmed Ally Salum akionesha Fomu baada ya kuchukua Fomu ya Maombi ya Kugombea Nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Solwa kupitia Chama Chama cha Mapinduzi (CCM) leo Juni 28,2025.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mbunge wa Jimbo la Solwa mkoani Shinyanga, Mhe. Ahmed Ally Salum, leo Juni 28, 2025, ameonesha nia ya kuendelea kulitumikia jimbo hilo kwa kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kugombea tena nafasi ya Ubunge katika uchaguzi mkuu ujao.
Mhe. Ahmed Salum, ambaye amekuwa Mbunge wa Jimbo la Solwa tangu mwaka 2005, ambapo mara baada ya kuchukua fomu, ameonekana mwenye furaha na matumaini makubwa ya kuendelea na dhamana hiyo ya kuwatumikia wananchi.
“Ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kutufikisha mpaka siku ya leo tukiwa wazima, lakini pia nakishukuru Chama Cha Mapinduzi kwa kuendelea kuniamini. Leo nimechukua fomu kwa nia ya kugombea kwa awamu nyingine tena Ubunge katika Jimbo la Solwa, kuteuliwa kugombea ni kitu kingine,chama kitafanya maamuzi ya nani anafaa kuwa mbunge wa Jimbo la Solwa”,amesema Ahmed Salum.

