Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Mazingira Prof. Peter Msoffe akisalimiana na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Bw. Paul Masanja alipowasili katika Ofisi hizo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo Juni 28, 2025.
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Mazingira Prof. Peter Msoffe akisaini kitabu ofisini kwa Katibu Mkuu alipowasili katika Ofisi hizo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo Juni 28, 2025.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na Menejimenti na watumishi wakati wa hafla ya mapokezi ya Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Mazingira Prof. Peter Msoffe alipowasili katika Ofisi hizo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo Juni 28, 2025.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja akimkabidhi nyaraka mbalimbali Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Mazingira Prof. Peter Msoffe alipowasili katika Ofisi hizo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo Juni 28, 2025.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Mazingira Prof. Peter Msoffe alipowasili katika Ofisi hizo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo Juni 28, 2025.
…….
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja amewaongoza viongozi na watumishi wa Ofisi hiyo katika mapokezi ya Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Mazingira Prof. Peter Msoffe aliyewasili Ofisi hizo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo Juni 28, 2025.
Akizungumza wakati wa hafla ya mapoke, Mhandisi Luhemeja pamoja na mambo mbalimbali amemkabidhi jukumu la kuhakikisha biashara ya kaboni kupitia bahari inachukua nafasi.
Amesema maeneo mbalimbali yakiwemo ya pwani ya bahari yamejaliwa kuwa na misitu ikiwemo mikoko ambayo inahitaji kutumiwa ipasavyo katika biashara ya kaboni.
Alimwomba Naibu Katibu Mkuu huyo kushirikana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia katika eneo la miradi ya kaboni kwa kuiunganisha na ajenda ya nishati safi ya kupikia hasa uhifadhi wa msiitu.
Alisema Wizara hiyo imefanya vizuri katika kutekeleza maelekezi ya Serikali ya kwa shule zake kuanza kutumia nishati safi na kuachana na kuni na mkaa hatua ambayo imechangia kuacha kukata miti na kuihifadhi kwa ajili ya biashara ya kaboni ambayo inawaingizia fedha.
“Mazingira ni sehemu ya kuisaidia nchi, tunayo misitu mingi lakini hatuitumii ipasavyo hivyo mwaka mpya wa fedha unaaonza uwe wa mabadiliko tunahitaji fedha hizi kutokana na biashara ya kaboni kwani mazingira ni uchumi,” alisema.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Prof. Msoffe alisema suala la mazingira liko moyoni kwa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan hivyo hatuna budi kuendelea kuyalinda.
Aliahidi kutoa ushirikiano akisema anatambua wajibu wa kila mmoja katika kuhakikisha wanaisaidia Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikia kulinda mazingira.
Pia, Prof. Msoffe alisema yuko tayari kupokea mawazo mapya ya ubunifu katika suala zima la hifadhi mazingira ambayo yatakuwa chachu katika maendeleo endelevu.Itakumbukwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Prof. Msoffe ambaye ameapishwa leo Juni 28, 2025 Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma, aliteuliwa kushika wadhifa huo akichukua nafasi ya Bi. Christina Mndeme.