Nkanwa Magina Meneja Uendeshaji Bodi ya Bima ya Amana akitoa maelezo kwa wageni mbalimbali waliotembelea banda la taasisi hiyo Leo Juni 30, 2025 katika maomesho ya 49 ya biashara ya kimataifa Sabasaba yanayoandaliwa na TANTRADE na kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere barabara ya Kilwa jinini Dar es Salaam
Bodi ya Bima ya Amana mwaka huu kama taasisi zingine nayo inashiriki kikamilifu katika maonesho hayo ili kuelimisha wananchi kuhusu shughuli zake.
Kauli Mbiu ya maonesho hayo ni “Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam ‘Sabasaba’ – Fahari ya Tanzania.”
Katika picha katikati ni Romuli Mtoi Mhasibu Mwandamizi Bodi ya Bima ya Amana.
Joyce Shala Afisa Mwandamizi Bodi ya Bima ya Amana akifafanua Jambo kwa mmoja wa wananchi waliotembelea banda la taasisi hiyo.
Nkanwa Magina Meneja Uendeshaji Bodi ya Bima ya Amana akijadiliana jambo na Romuli Mtoi Mhasibu Mwandamizi Bodi ya Bima ya Amana wakiwa tayari kabisa kuwahudumia wananchi mbalimbali wanaotembelea katika banda Hilo kwenye maonesho ya Sabasaba viwanja vya Julius Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Joyce Shala Afisa Mwandamizi Bodi ya Bima ya Amana akifafanua Jambo kwa wananchi waliotembelea banda la taasisi hiyo.
Beatrice Hyera Afisa Mwandamizi Bodi ya Bima ya Amana akiwasikiliza baadhi ya wananchi waliotenbelea katika banda la Bodi ya Bima ya Amana ili kupata elimu kuhusu shughuli za bodi Hi you.