Na Mwandishi Wetu
KADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kibada Wilaya ya Kigamboni Dkt.Nazar Kirama amerudisha fomu ya kuomba ridhaa ya chama cha Mapinduzi kugombea Ubunge Jimbo la Kigamboni kwa kipindi cha mwaka 2025/2030.
Kada huyo amesema kwa sasa kazi iliyobaki ni kufanya operesheni ya mtu kwa mtu, nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa kuhakikisha kuwa Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi wa Octoba, Dk. Samia Suluhu Hassani anapata kura 100%
Kirama ,amerudisha fomu hiyo katika ofisi ya Wilaya ya CCM Kigamboni.
Kirama amebainisha kwamba yeye yupo tayari kushirikiana na yeyote atakayeteuliwa na vikao vya juu vya CCM baada ya mchujo. Pia Dr.Kirama amesema kuwa yeye kama kada wa CCM anachoangalia na kilichopo kwenye maono yake baada ya mchujo ni mustakabali wenye nguvu na afya wa chama chake cha CCM katika eneo la Wilaya ya Kigamboni. Baada ya zoezi la mchujo na kura za maoni nitashikiana 100 kwa 100 yule atakaye teuliwa na CCM kupeperusha bendera ya CCM katika jimbo la Kigamonio.
Aidha amesema ametumikia nafasi mbalimbali ndani ya Chama hivyo ana uzoefu wa kuweza kuwatumikia wananchi wa Kigamboni .