Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa ameshika mfano wa funguo kuashiria uzinduzi wa Benki ya Maendeleo kuwa Benki kamili ya Biashara pamoja, mpango mkakati wa miaka mitano Huduma M-Bank, iliyofanyika katika ukumbi wa Hyatty Regency jijini Dar es Salaam Julai 3, 2025. Kutoka kushoto ni Mkuuwa Wilaya Ilala Edward Mpogolo, Naibu Waziri wa Fedha Hamad Chande, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Lomnyaki Saitabau na Mwakilishi wa Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT Dean Chadiel Lwiza. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikabidhiwa Tuzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Lomnyaki Saitabau ya kutambua na kuthamini mchango wake katika ukuaji na mafanikio ya Benki ya Maendeleo Plc, kwenye Hafla ya uzinduzi wa Benki ya Maendeleo kuwa Benki kamili ya Biashara pamoja na mpango mkakati wa miaka mitano, iliyofanyika katika ukumbi wa Hyatty Regency jijini Dar es Salaam Julai 3, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza kwenye Hafla ya uzinduzi wa Benki ya Maendeleo kuwa Benki kamili ya Biashara pamoja na mpango mkakati wa miaka mitano, iliyofanyika katika ukumbi wa Hyatty Regency jijini Dar es Salaam Julai 3, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
β¦β¦β¦
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali itaendelea kuimarisha mazingira ya ufanyaji biashara za huduma za kifedha ili kuvutia uwekezaji wa ndani na nje kwa kuwa maendeleo endelevu ya taifa hayawezi kufikiwa bila ushiriki thabiti wa sekta binafsi.
Amesema kuwa sekta ya fedha ni kichocheo kikubwa katika ukuaji wa Uchumi na ustawi wa wananchi kwa ujumla na ni moja ya sababu inyowezesha maendeleo ya Taifa kwenda kwa kasi.
Amesema hayo leo Alhamisi (Julai 03, 2025) wakati wa uzinduzi wa Benki ya Maendeleo PLC, kuwa Benki kamili ya kibiashara, kwenye ukumbi wa mikutano wa hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
βEndeleeni kuimarisha ushirikiano miongoni mwenu, serikali kwa kutambua umuhimu wa sekta ya fedha katika kuchagiza maendeleo, imeendelea kuhamasisha matumizi ya teknolojia bunifuβ.
Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa taasisi zote za kifedha zikiwemo benki kuongeza juhudi katika kutoa elimu ya kifedha kwa wananchi ili kuwajengea uwezo wa kuelewa, kutumia na kunufaika na huduma za kifedha kwa maendeleo yao binafsi na kwa ustawi wa taifa kwa ujumla.
βTukifanya haya tutapunguza wizi, upotevu wa fedha kiholela kwa sababu kila mmoja atakuwa anaweza kujua fedha yake ataipataje, ataihifadhi wapi na namna ya kutoa lakini pia wapeni wateja wenu namna ya utunzaji wa fedhaβ
Pia, Mheshimiwa Majaliwa ameongeza kuwa kwa mujibu wa takwimu za utafiti wa Finscope huduma jumuishi za fedha zimeweza kukua kutoka asilimia 65 mwaka 2017 hadi kufikia asilimia 76 mwaka 2023. βkwa mujibu wa utafiti huo, matumizi ya huduma za benki yameongezeka na kufikia asilimia 22 mwaka 2023 kutoka asilimia 17 mwaka 2017β.
Kadhalika, Mheshimiwa ametoa wito kwa taasisi zote za fedha zijenge mifumo rahisi na rafiki kwa makundi yote ya watumiaji wa huduma za kifedha.
Awali, Akizungumza kwa niaba ya Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT na Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dkt. Alex Malasusa, Muwakilishi wa Askofu Dean Chadiel Lwiza ameishukuru Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa kuisimamia benki hiyo na kuwa mfano wa benki iliyoanzishwa na wazawa kwa mtaji mdogo hadi kufikia kuwa benki kitaifa. βTunaiomba benki kuu jicho lenu liwe kali kuliko letu, itazameni hii benkiβ
Kadhalika, ameongeza kuwa sera nzuri na mazingira mazuri ya uwekezaji katika biashara na usimamizi mzuri za biashara. βTunaishukuru Serikali ya awamu ya Sita inayoomgizwa na Rais Dkt. Samia kwa kuendelea kuweka mazingira haya mazuri ya ufanyaji biasharaβ
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank PLC Lomnyaki Saitabau amesema kuwa benki hiyo imejiweka katika nafasi bora zaidi ya kuwa benki ya kisasa, shindani na jumuishi kwa Watanzania wote hasa kipindi dunia inapoelekea kwenye zama mpya zenye msukumo wa kiteknolojia, ubunifu, na uwajibikaji wa hali ya juu.
βKwa kufanya hivyo, tunaunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Dkt.Β Samia Suluhu Hassani, yenye dhamira ya kuwafikia watanzania wengi zaidi nchi nzima kupitia dira ya taifa ya ujumuishaji wa kifedha (financial inclusion) na kuchochea maendeleo ya kiuchumi kupitia sekta binafsi, tutaendelea kushirikiana na Serikali, katika ujenzi wa Uchumi wa nchiβ.
Naye, Naibu Waziri wa Fedha Hamad Hassan Chande ameipongeza benki hiyo kwa hatua kuwa iliyofikiwa na benki hiyo katika utoaji huduma kwa watanzania hasa kwa kutumia fursa zilizowekwa na Serikali βSisi Wizara ya Fedha tumeendelea kuweka mazingira mazuri na rafiki ya ufanyaji wa shughuli za kifedha, sasa wekeni mkakati wa kuifikisha benki hii maeneo mengi zaidiβ.
βΒ