Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Bi. Latifa Khamis, akiongozwa na Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Fedha, Bw. Ramadhan Kissimba, kutembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

Katibu Mtendaji wa Mamlaka ya Rufani za Zabuni za Umma, CPA James Sando, akiongozwa na Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Fedha, Bw. Ramadhan Kissimba, kutembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

Afisa kutoka Idara ya Uchambuzi wa Sera Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Fronto Furaha, akimkabidhi Kiongozi wa ujumbe wa Shirika la World Vision Tanzania Mkoa wa Tanga wa mradi wa utunzaji mazingira, Bw. Swalehe Mwachuo machapisho yanayohusu Sera, walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

Afisa kutoka Idara ya Uchambuzi wa Sera Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Fronto Furaha, akitoa elimu ya Sera za Fedha na Uchumi kwa Ujumbe wa Shirika la World Vision Tanzania Mkoa wa Tanga wa mradi wa utunzaji mazingira, ukiongozwa na Bw. Swalehe Mwachuo ulipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

Ujumbe wa Shirika la World Vision Tanzania Mkoa wa Tanga wa mradi wa utunzaji mazingira, ukiongozwa na Bw. Swalehe Mwachuo ukionesha machapisho mbalimbali waliyopewa walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

Afisa Mwandamizi kütoka Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Bi. Mary Mihigo, akitoa elimu ya fedha kuhusu riba, mikopo na uwekezaji kwa Ujumbe wa Shirika la World Vision Tanzania Mkoa wa Tanga wa mradi wa utunzaji mazingira, ukiongozwa na Bw. Swalehe Mwachuo, ulipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

Afisa Mwandamizi kitika Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Bi. Mary Mihigo, akitoa elimu ya fedha kuhusu usajili kwa watoa huduma ndogo za fedha kwa Bw. Samson Joel, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

Afisa Mwandamizi kutoka Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Bw. Sepo Seni, akitoa elimu kwa Bw.Canute Hyandye, kuhusu Deni la Serikali na Deni la Taifa, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha).
…….
Na. Peter Haule na Joseph Mahumi ,WF, Dar es Salaam
Wizara ya Fedha imeendelea kupongezwa kwa utoaji wa elimu yenye uhalisia na maisha ya wananchi katika masuala ya fedha na uchumi kwa kutumia fursa zilizopo na matumizi bora ya fedha katika kuchochea maendeleo.
Hayo yameelezwa na ujumbe wa Shirika la World Vision Tanzania Mkoa wa Tanga wa mradi wa utunzaji mazingira, ukiongozwa na Bw. Swalehe Mwachuo, ulipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Bw. Mwachuo alisema kuwa wamevutiwa na elimu kuhusu Sera za Fedha na elimu ya huduma ndogo ya fedha ambayo inauhalisia kwa wajumbe wengi wa mradi huo na maeneo walikotoka.
Alisema kuwa, ujumbe uliotembelea Banda la Wizara ya Fedha umetoka Mkoani Tanga katika Wilaya za Mkinga, Pangani, Handeni na Kilindi ambao umekuja kupata elimu ya kazi zinazofanywa na Wizara ya Fedha hususani zilizo na manufaa ya moja kwa moja kwa wajumbe hao.
Alisema wajumbe hao watapeleka taarifa kwa wananchi wengine kuhusu Sera za fedha na namna ya kuepukana na mikopo umiza, kukopa kwa malengo na kutotumia fedha za mikopo kwenye matumizi yasiyo na faida.
Bw. Mwachuo alisema kuwa wamejifunza kuwa fedha za mkopo sio za mkopaji bali faida ndio ya mkopaji hivyo ni vema kutumia fedha ya mkopo kuzalisha ili kupata faida.
Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha kupitia Idara na Vitengo lakini pia Taasisi zilizo chini ya Wizara, wanaendelea kuwakaribisha watanzania kufika katika Banda la Wizara hiyo ili waweze kuwahudumia.