NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika viwanja hivyo, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Mabele, ameeleza kuwa ushindi huo ni ishara ya uwezo mkubwa wa vijana wa Kitanzania waliopitia mafunzo ya kijeshi na ya uzalishaji kupitia JKT.
“Tunawaalika wananchi wote kutembelea banda letu ili kujionea huduma mbalimbali tunazotoa, zikiwemo huduma za ulinzi wa kidijitali, mavazi, maji ya Uhuru, pamoja na bidhaa nyingine zenye ubora wa hali ya juu zilizotengenezwa na vijana wetu,” amesema Meja Jenerali Mabele.
Ameongeza kuwa JKT inaendelea kuwa sehemu ya muhimu ya Maonesho haya kila mwaka, na imedhihirisha kuwa vijana wanaopitia mafunzo ya kijeshi siyo tu watendaji wa ulinzi, bali pia ni wataalamu wa kazi za uzalishaji na ubunifu unaochangia pato la taifa.
Meja Jenerali Mabele pia amesisitiza kuwa mafanikio haya ni matokeo ya uwekezaji katika mafunzo ya stadi za kazi na nidhamu kwa vijana, huku akisisitiza dhamira ya JKT ya kuendelea kuwajengea vijana uwezo wa kujitegemea na kuchangia katika maendeleo ya Taifa.








