Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda akizungumza wakati wa ufunguzi wa programu ya Samia Extended Scholarship DS/AI+ katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Julai 8,2025 jijini Arusha.
……
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amezindua rasmi programu ya Samia Extended Scholarship DS/A+, inayolenga kufadhili wanafunzi wa Tanzania bara na Zanzibar kusoma katika Vyuo Vikuu mahiri duniani, katika fani za kimkakati za Sayansi ya Data, Akili Unde (Artificial Intelligence), na Sayansi Shirikishi kwa mwaka wa masomo 2025/2027.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika Julai 8, 2025 jijini Arusha, Prof. Mkenda alieleza kuwa, mpango huo unalenga kuwanufaisha wanafunzi 50 waliobobea katika tahasusi za sayansi asilia zenye hisabati ya juu (advanced mathematics). Alibainisha kuwa waombaji watakaofanikiwa watahitajika kushiriki Kambi ya Kitaifa ya Maarifa kwa muda wa miezi kumi (10) katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) kabla ya kuanza masomo yao nje ya nchi.
Prof. Mkenda alisisitiza kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejipanga kuwekeza kwa dhati katika maendeleo ya sayansi, teknolojia na ubunifu kwa ajili ya maendeleo ya taifa. Alitoa wito kwa vijana kutumia fursa hiyo kwa bidii na maarifa ili kuchochea mageuzi ya kisayansi na kiteknolojia nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt. Amos Nungu, amesema Programu ya Samia Extended Scholarship (DS/A+) inatekelezwa kwa hatua tatu, ambapo ya kwanza inahusisha kambi ya kitaifa ya maarifa kwa miezi kumi ili kuwapa vijana mafunzo ya uzalendo, maadili ya kitaifa na mawasiliano ya kimataifa.
Dkt. Nungu alieleza kuwa, hatua ya pili ni maandalizi ya kisaikolojia kwa vijana kabla ya kusoma nje ya nchi, huku hatua ya tatu ikitoa ufadhili wa masomo ya Uzamili katika Sayansi ya Data na Akili Unde kupitia ushirikiano na Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela NM-AIST
na IIT Madras Zanzibar.
Makamu Mkuu wa Taasisi ya NM-AIST, Prof. Maulilio Kipanyula, amesema taasisi yao imejiandaa kikamilifu kutoa mazingira bora ya mafunzo ili kuwajengea wanufaika maarifa na ujuzi wa kisasa.
Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Programu hiyo, Prof. Makenya Maboko, ameishukuru Serikali kwa kuanzisha mpango huo unaowawezesha vijana wa Kitanzania kujifunza taaluma za sayansi kama data, hatua ambayo itaisaidia nchi kuendana na maendeleo ya teknolojia na kukuza uchumi.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda akizungumza wakati wa ufunguzi wa programu ya Samia Extended Scholarship DS/AI+ katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Julai 8,2025 jijini Arusha.
Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula akitoa neno la utangulizi wakati wa ufunguzi wa programu ya Samia Extended Scholarship DS/AI+ Julai 8,2025 jijini Arusha .
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kituo cha Tehama Rasimali (ICT-RC) katika Taasisi ya NM-AIST Dr. Devotha Nyambo wakati wa ufunguzi wa programu ya Samia Extended Scholarship DS/AI+ Julai 8,2025 jijini Arusha.
Waziri Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda akiwa katika studio ya Nelson Mandela Fm na Kituo cha Mafunzo Kidigitali wakati wa ufunguzi wa programu ya Samia Extended Scholarship DS/AI+ Julai 8,2025 jijini Arusha.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda ( kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof Maulilio Kipanyula mara baada ya ufunguzi wa programu ya Samia Extended Scholarship DS/AI+ julai 8,2025.
Washiriki wa ufunguzi wa programu ya Samia Extended Scholarship DS/AI+ wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa ufunguzi wa programu hiyo katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Julai 8,2025 jijini Arusha.
Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa ufunguzi wa programu ya Samia Extended Scholarship DS/AI+ Julai 8,2025 Jijini Arusha.