Mkurugenzi wa Taasisi ya Miriam Odemba Foundation (MOF) ambaye pia ni mwanamitindo nguli wa kimataifa, Miriam Odemba amesisitiza Watanzania kuchangia fedha kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa vyoo na baadhi ya miundombinu katika Shule ya Misingi Mwendapole iliyopo Kibaha mkoani Pwani.
Hatua hiyo ni juhudi za taasisi hiyo katika kuiunga mkono serikali kuhakikisha wanafunzi wanapata miundombinu bora na imara ya kujisomea.
Odemba amefafanua kauli hiyo, akisema kuwa lengo mojawapo la taasisi yake ni kuhakikisha vyoo vipya zaidi ya 14 vinakamilika, na vingine vitaendelea kukarabatiwa kwa awamu, ikihusisha jumla ya vyoo 36, na miundombinu mingine.
Shule hiyo imekuwa ikiteseka kwa miaka kadhaa sasa kwa changamoto za miundombinu, zinazopelekea binti wa kike kusoma kwenye mazingira magumu.
“Kutuunga kwako mkono ni muhimu, kwani hakuna mchango mdogo wowote unahitajika kufanikisha hili,” amesema Miriam.
Taasisi hiyo imekuwa ikijishughulisha kwa ajili ya kumjengea mazingira wezeshi kwa binti wa kike nchini kusoma na kupanga malengo yake ya baadae, na pia kuchangia maboresho kwenye sekta mbalimbali, ikiwemo urembo, vipaji, sanaa na Elimu.
“Sisi tuna upendo, na tunatamani watanzania wote tuungane kwa pampja katika kuleta mabadiliko chanya kwa ajili ya jamii yetu.” alisisitiza Miriam.
Miriam amewaomba watanzania wenye Moyo Jl kuchangia kwa njia ya Simu hata kiasi cha Tshs. 1000 au zaidi kwa namba 0749 808073 jina litatokea MIRIAM ODEMBA FOUNDATION au kwa Benki ya NBC Acount Namba 011172000038