Washindi wa jumla wa maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa kampuni ya GF Trucks & Equipment’s ltd, imesherehekea ushindi huo kwa staili ya aina yake kwa kujumuisha Wadau na wafanyakazi wa kampuni hiyo pamoja na wateja katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es salaam.
Kufuatia ushindi wa jumla uongozi wa kampuni hiyo,uliwakutanisha pamoja wafanyakazi wa kiwandani na wateja wao ambao ndio nguzo yao katika kuelekea mafanikio.
Akizungumza wakati wa sherehe hiyo mwenyekiti wa bodi ya Wakurugezi ya kampuni ya GF, Mehboob Karmali alisema mafanikio hayo yametokana na mazingira mazuri ya serikali kwa wawekezaji na wao kama uongozi wametengeneza Utatu (3) Uongozi ,wafanyakazi na serikali huu utatu ndio siri ya mafanikio yetu Pia alisema GF inauza magari aina zoote kuanzia madogo hadi makubwa akwa ajili yaa shughuli za migodini na kilimo
Brand ya FAW ,XCMG,Mahindra na Hyundai ni miongoni mwa magari na mitambo inayopatikana katika kampuni hiyo na chakujivunia magari hayo yanaunganishwa katika kiwanda cha GF Vehicle Assemblers (GFA) kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
Nae Meneja wa kiwanda hicho , Ezra Mereng aliupongeza uongozi mzima wa kampuni hiyo,wafanyakazi na kampuni hiyo kwa jitihada za dhati kuhakikisha wanapambanaa na kuuza bidhaa kutoka nyumban,i pia kutokana na uongozi imara na serikali kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji katika sekta ya magari basi tutarajie makubwa .
.jpeg)
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugeni ya kamapuni ya GF Trucks , Mehboob Karmali (katikati)akifurahi kwa pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo pamoja na viongozi wakati wa ahafla ya kusherehekea ushindi wa ajumla wa amaonyesho ya sabasa 2025