Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Kenan Kihongosi wakati akiwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kwaajili ya kufungua Mkutano wa 14 wa Kimataifa wa Watunga Sera wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii Barani Afrika. Tarehe 10 Julai 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati akiwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kwaajili ya kufungua Mkutano wa 14 wa Kimataifa wa Watunga Sera wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii Barani Afrika. Tarehe 10 Julai 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Viongozi mbalimbali wakati akiwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kwaajili ya kufungua Mkutano wa 14 wa Kimataifa wa Watunga Sera wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii Barani Afrika. Tarehe 10 Julai 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati akikagua mabanda mbalimbali ya Taasisi za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii katika Mkutano wa 14 wa Kimataifa wa Watunga Sera wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii Barani Afrika unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC). Tarehe 10 Julai 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akitoa maelekezo kwa Viongozi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuhusu kuzingatia wananchi ambao wapo katika sekta zisizo rasmi wakati akikagua mabanda mbalimbali katika Mkutano wa 14 wa Kimataifa wa Watunga Sera wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii Barani Afrika unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC). Tarehe 10 Julai 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati wa Mkutano wa 14 wa Kimataifa wa Watunga Sera wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii Barani Afrika unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC). Tarehe 10 Julai 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikabidhiwa tuzo kwaajili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyotolewa na Jumuiya ya Hifadhi ya Jamii Barani Afrika (ASSA) wakati wa Mkutano wa 14 wa Kimataifa wa Watunga Sera wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii Barani Afrika unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) leo tarehe 10 Julai 2025. Anayekabidhi ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa Mataifa mbalimbali ya Afrika wanaoshiriki Mkutano wa 14 wa Kimataifa wa Watunga Sera wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii Barani Afrika unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC). Tarehe 10 Julai 2025.
………
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema pamoja na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Barani Afrika kutumika kuwekeza katika kuendeleza miundombinu ni vema kuhakikisha michango ya wanachama ambayo imetengwa kama kinga dhidi ya misukosuko ya kiuchumi na kijamii pamoja na kukabiliana na umaskini inabaki kuwa ya kutosha kukidhi malengo ya msingi ya uanzishwaji wake.
Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akifungua Mkutano wa 14 wa Kimataifa wa Watunga Sera wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii Barani Afrika unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC). Amesisitiza kuwepo umakini kwenye uwekezaji wa miradi ya miundombinu kwani miradi ambayo haiwezi kutekelezeka inaweza kudhoofisha uwezo wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kutimiza wajibu wake.
Aidha Makamu wa Rais amesema ni muhimu tahadhari ichukuliwe ili kuepusha miradi iliyobuniwa vibaya, yenye gharama kubwa kupita kiasi au miradi migumu kupita kiasi ambayo ni ngumu kuisimamia na ile isiyokidhi mahitaji ya walengwa wa mifuko ya hifadhi ya jamii. Ameongeza kwamba iwapo upembuzi yakinifu na thabiti wa miradi ya miundombinu hautafanywa mapema inaweza kusababisha kuchelewa kwa malipo ya walengwa au hata kushindwa kabisa kuirejesha.
Vilevile Makamu wa Rais amewahimiza wataalamu wanaohudhuria mkutano huo kuandaa mikakati ya jinsi gani Mifuko bora ya Hifadhi ya Jamii inaweza kuchangia katika kuongeza juhudi zinazoendelea za kuongeza ufadhili wa uwekezaji katika miundombinu ya kijamii na kiuchumi maeneo ya vijijini. Amesema uwekezaji katika miundombinu ya vijijini utasaidia kuongeza tija na ubora wa maisha katika maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji, kutengeneza ajira na kupunguza uhamaji wa wananchi kutoka vijijini kwenda mijini.
Makamu wa Rais amesema ufadhili wa miundombinu Barani Afrika unakadiriwa kuwa na upungufu kati ya dola bilioni 68 -108 kila mwaka hali inayopelekea wachambuzi wengi wa maendeleo kukubaliana kwamba Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ipo katika nafasi nzuri ya kufanya kazi zaidi kama chachu ya kuharakisha maendeleo ya miundombinu barani Afrika kwa kuondoa upungufu huo wa ufadhili.
Amewahimiza Watunga Sera wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii Barani Afrika wanaoshiriki katika mkutano huo kutoa mawazo ya vitendo na masuluhisho kuhusu namna ambavyo Mifuko ya Hifadhi ya Jamii inaweza kutekeleza jukumu la ufadhili katika miundombinu vyema na kwa uendelevu.
Mkutano huo umehudhuriwa na Viongozi mbalimbali kutoka Mataifa ya Afrika ikiwemo Mawaziri na Wataalamu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Kauli mbiu ya mkutano huo ni “Mifuko ya Hifadhi ya Jamii: Chachu ya Maendeleo ya Miundombinu na Ukuaji wa Kiuchumi na Kijamii Barani Afrika.”