TAARIFA KWA UMMA
Jeshi la Polisi lingependa kutoa ufafanuzi kuhusu madai ya Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo kwamba wamemwandikia barua Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini kutokana na madai ya Viongozi wao kuwa wametakiwa kuwasilisha taarifa na majina ya watia nia ya kugombea ubunge na udiwani kwa Jeshi la Polisi.
Barua hiyo haijamfikia Mkuu wa Jeshi la Polisi na endapo itamfikia maudhui yake yatafanyiwa kazi kwa haraka ili kupata ukweli wake na mawasiliano hayo yametoka wapi na yametolewa.