Kamishna Idara ya Michezo Zanzibar Ameir Mohammed Makame na Wadau kutoka Taasisi mbalimbali ikiwemo ZAWA, ZECO, ZIMAMOTO na Zimamoto wakikaguwa viwanja vya Maozedong Wilaya ya Mjini.
…….
Kamishna Idara ya Michezo Zanzibar Ameir Mohammed Makame amewataka Wadau wa michezo kuwa wastahamilivu na kuiacha Serikali kutekeleza mipango ya maendeleo iliojipangia.
Ameyasema hayo mara baada ya kumalizika kwa ukaguzi wa viwanja vya Mao zedong Wilaya ya Mjini.
Amesema baadhi ya Wanadau wa Michezo wakitumia mitandao ya kijamii, kuipaka matope Serikali kupitia Idara ya Michezo kwa madai ya kutofunguliwa viwanja hivyo hadi sasa.
Aidha Kamishna Ameri, amesema suala hilo ni la kisheria na kitaalamu hivyo amewataka Wanamichezo, Wadau wa Michezo na Wananchi kwa ujumla kusubiri taratibu zilizowekwa zikamilike.
Hata hivyo amesema baada ya kuridhishwa na ukaguzi, watafanya makabidhiano na baadae kupangwa kwa ajili ya matumizi.
Kwa upande wake Mshauri elekezi kutoka AE&Q Consultant limited Mhandisi Feisal Fadhili Sudy amesema ujenzi wa Mradi huo, umefikia asilimia 99 na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo madogo madogo yaliopo ikiwemo Genereta na Internat.
Hata hivyo ameiipongeza Serikali kupitaia Wizara ya Hbari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa mashirikiano makubwa waliotoa wakati wa ukarabati wa viwanja hivyo.
Ukaguzi wa viwanja hivyo, umeshirikisha Taasisi mbali mbali ikiwemo watendaji wa Idara ya Michezo, Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), Mamlaka ya kukabiliana na Maafa na Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar.