WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mhe. George Simbachawene akizungumza leo Julia 11,2025 jijini Dodoma ,wakati akifungua Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika,yakiongozwa na kauli mbiu ya kukuza na kulinda heshima ya binadamu katika mapambano dhidi ya Rushwa.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Chrispin Chalamila,akizungumza wakati akifungua Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika,yakiongozwa na kauli mbiu ya kukuza na kulinda heshima ya binadamu katika mapambano dhidi ya Rushwa.

Mwakilishi wa Bodi ya Ushauri ya Masuala ya Rushwa ya Umoja wa Afrika,Benjamin Kapera,akizungumza wakati akifungua Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika,yakiongozwa na kauli mbiu ya kukuza na kulinda heshima ya binadamu katika mapambano dhidi ya Rushwa.

Mkurugunzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa uchumi Zanzibar (ZAECA) Bw.Ali Abdalla Ali,akizungumza wakati akifungua Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika,yakiongozwa na kauli mbiu ya kukuza na kulinda heshima ya binadamu katika mapambano dhidi ya Rushwa.


SEHEMU ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika,yakiongozwa na kauli mbiu ya kukuza na kulinda heshima ya binadamu katika mapambano dhidi ya Rushwa.


SEHEMU ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika,yakiongozwa na kauli mbiu ya kukuza na kulinda heshima ya binadamu katika mapambano dhidi ya Rushwa.


SEHEMU ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika,yakiongozwa na kauli mbiu ya kukuza na kulinda heshima ya binadamu katika mapambano dhidi ya Rushwa.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof.Palamagamba Kabudi,akitoa mada wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika,yakiongozwa na kauli mbiu ya kukuza na kulinda heshima ya binadamu katika mapambano dhidi ya Rushwa.
Na.Meleka Kulwa-DODOMA
WAZIRI wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika jitihada za kutokomeza rushwa, ikiwa ni pamoja na kutunga na kufanya maboresho ya sheria mbalimbali zinazolenga kupambana na vitendo hivyo.
Miongoni mwa sheria alizozitaja ni pamoja na Sheria ya Fedha ya Umma, Sheria ya Kudhibiti Fedha Haramu, Sheria ya Mashitaka, Sheria ya Ukaguzi wa Fedha ya mwaka 2008, Sheria ya Kudhibiti Matumizi ya Fedha Wakati wa Uchaguzi ya mwaka 2010, Sheria ya Kulinda Watoa Taarifa na Mashahidi ya mwaka 2015, Sheria ya Upatikanaji wa Taarifa ya mwaka 2016, na Sheria ya Uhujumu Uchumi iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2016.
Waziri Simbachawene ameyasema hayowakati akifungua Kongamano la maadhimisho ya siku ya mapambano dhidi ya rushwa barani Afrika yaliyofanyika leo Julai 11,2025 jijini Dodoma.
Amesema kuanzishwa kwa Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ndani ya Mahakama Kuu pamoja na Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2023 ni hatua nyingine muhimu katika kuhakikisha kwamba vitendo vya rushwa vinadhibitiwa ipasavyo.
Waziri Simbachawene ameeleza kuwa Mkataba wa Umoja wa Afrika wa Kupambana na Rushwa umeweka misingi ya nchi wanachama kushirikiana katika mafunzo, sheria, na mikakati ya kuzuia na kupambana na rushwa kwa pamoja.
“Kupitia mkataba huo, nchi zimewekewa wajibu wa kushughulikia kwa haraka maombi ya vyombo vya dola vinavyohusika na upelelezi, mashitaka, na utoaji wa adhabu kwa watuhumiwa wa makosa ya rushwa na yale yanayohusiana nayo.”Amesema Simbachawene.
“Marekebisho ya sheria yaliyofanyika mwaka 2024 yameongeza nguvu zaidi kwa kutambua makosa ya rushwa yanayofanyika katika chaguzi, burudani, michezo pamoja na michezo ya kubahatisha.”Amesema.
Mhe.Simbachawene amesema kupitia Sheria ya Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007, TAKUKURU imepewa mamlaka ya kuhakikisha kuwa rushwa inatokomezwa nchini, na serikali imeendelea kuipatia rasilimali fedha, kibali cha kuajiri watumishi wapya, pamoja na vitendea kazi na samani za ofisi ili kuongeza ufanisi wake.
“Natoa wito kwa wadau wote kuja na mbinu mpya ambazo hazijazoeleka ili kusaidia kuboresha mapambano dhidi ya rushwa. Tunapaswa kuangalia namna taasisi zetu zinavyohudumia wananchi, kwani huduma bora na haki ni kipimo muhimu cha mafanikio yetu,” alisema Simbachawene.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Chrispin Chalamila,amesema kuwa rushwa ni kikwazo kikubwa kwa ustawi wa wananchi na inachangia kuwepo kwa vitendo vingine vya kidhalimu ambavyo vimekatazwa katika katiba ya Tanzania.
Bw.Chalamila amesema kuwa jitihada za kuendelea kuimarisha mapambano dhidi ya Vitendo vya rushwa zitachangia kufikia lengo la Serikali la kuleta ustawi wa jamii ya watanzania na kukuza heshima ya ubinadamu.
“Majadiliano kuhusu rushwa yanayofanyika katika maadhimishoo hayo yatasaidia kukuza heshima ya binadamu barani Afrika,ambapo mara nyingi huchukuliwa haki zao kutokana na vitendo vya rushwa”ameongeza
Naye Mkurugunzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa uchumi Zanzibar (ZAECA) Bw.Ali Abdalla Ali,ameseam kuwa maadhimisho hayo yatasaidia kufikisha ujumbe kwa jamii kuhusu umuhimu wa kutojihusisha na vitendo vya rushwa na uhujumu uchumi nchini.
“Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni kukuza na kulinda heshima ya binadamu katika mapambano dhidi ya rushwa,ikizikumbusha taasisi zinazoratibu mapambano dhidi ya rushwa katika nchi wanachama wa umoja wa Afrika kulinda utu na haki za kila mtu ili kuimarisha utawala bora”amesema Bw.Ali
Mwakilishi wa Bodi ya Ushauri ya Masuala ya Rushwa ya Umoja wa Afrika,Benjamin Kapera,ametoa wito kwa Serikali za Afrika kuwekeza katika matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) ili kuhakikisha uwajibikaji na utoaji wa huduma kwa usawa.
akitoa mada katika Kongamano hilo,Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof.Palamagamba Kabudi amesisitiza umuhimu wa heshima ya binadamu kama haki ya msingi inayotambuliwa na mikataba ya kimataifa pamoja na katiba ya nchi.
Amesema kuwa uwepo wa rushwa katika jamii unavuruga misingi ya haki,usawa na utu wa binadamu na kwamba rushwa inapozidi watu hukosa huduma zinazostahili.
“ILi kukuza na kulinda heshima ya binadamu,ni muhimu kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa kwa njia madhubuti,shirikishi na endelevu”amesisitiza