Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, bi Fatma Hamad Rajab ametia Saini Hati ya Makubaliano (MOU) na Kampuni Haryana State Electronics Development Corporation (Hartron) ya Nchini India, kwa ajili ya kuwasaidia Vijana wa Zanzibar kupata mafunzo na vifaa, makubaliano ambayo yamefanyika huko Ukumbi wa Wizara hiyo, Migombani Mjini.
………….
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imetiliana saini hati ya Makubaliano (MOU) na Campuni ya Haryana State Electronics Development Corporation (Hartron) ya Maryana Nchini India kwa ajili ajili ya kuendeleza Vijana wa Zanzibar.
Utiaji Saini huo, umefanywa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, imetiwa saini na Katibu Mkuu wake bi Fatma Hamad Rajab na kwa upande wa Kampuni ya Harton, imetiwa saini na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Dk. Ganesan Jagadesan.
Viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo walihudhuria na Balozi wa India Nchini na Ujumbe wake ambao ulifanyika katika Ukumbi wa Wizara hiyo Migombani Wilaya ya Mjini.
Akizungumza katika Utiaji Saini wa Makubaliano hayo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Vijana, Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajab amesema lengo ni kusaidia Vijana, kupata mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) na Vifaa mbalimbali.
Aidha amesema hali hiyo itatoa fursa mbalimbali kwa vijana ikiwemo kuwaunganisha pamoja, kupata ajira na kuweza kufanya kazi kwa Ufanisi.
Kwa uapande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Haryana State Electronics Development Corporation kutoka India Dk. Ganesan Jagadesan ameahidi kufuata maelekezo yalimo katika Mkataba huo wa Maridhiano ili kuwasaidia Vijana wa Zanzibar.