Baadhi ya Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri wamesema diski mweko(Flash Disk) zilizowekewa maudhui ya elimu ya Afya zina mchango mkubwa katika kuleta mabadiliko ya tabia kwenye jamii ili kuzingatia kanuni za afya.
Wamebainisha hayo Mkoani Dodoma kwa nyakati tofauti mara baada ya Wizara ya Afya, Idara ya Kinga, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma kutoa zaidi ya diski mweko(Flash Disk) 600 kutolewa kwa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kwenye Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu hao.
Waganga wakuu hao wamesema maudhui yaliyopo katika Flashi hizo yana mchango mkubwa ambapo itarahisisha mwananchi kupata elimu ya afya kupitia TV pindi anaposubiria huduma katika vituo vya kutolea huduma za afya na maeneo mbalimbali yenye mkusanyiko wa watu.
Dkt.Catherine Saguti ni Mganga Mkuu Halmauri ya Mjini Kibaha amesema maudhui yaliyomo katika Flashi hizo yatasaidia sana kwa wananchi .
“Masomo yaliyopo kwenye flashi hizi yatasaidia sana ngazi ya vituo vya kutolea huduma za afya na kwenye jamii”amesema.
Mganga Mkuu Mkoa wa Tabora Dkt. Honoratha Rutabisibwa amesema jumbe zilizomo katika flashi hizo zitasaidia katika elimu ya afya kwenye jamii kwa nyanja tofauti ikiwemo huduma za uzazi,lishe .
Naye Mganga Mkuu Mkoa wa Mara Dkt. Zabron Masatu amesema katika mkoa huo Tv zimesambazwa katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma za afya hivyo wananchi wanapokwenda kupata huduma za afya hunufaika pia na elimu ya afya kupitia tv