BALOZI wa Tanzania nchini Comoro, Mhe. Saidi Yakubu akiwa katika mazungumzo na Rais wa nchi hiyo, Mhe. Azali Assoumani walipokutana hivi karibuni. Rais Azali amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ujio wake nchini Comoro na maelezo mazuri kwa wananchi na Serikali ya Comoro ambapo pamoja na mambo mengine, aliahidi kufanya kazi na Serikali ya Rais Azali kuimarisha Sekta ya Afya na kueneza lugha ya Kiswahili.