Na Humphrey Shao
GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Emmanuel Tutuba amesema miamala ya kifedha ya kidigitali imeongezeka zaidi ya milioni 500 kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2025/26 ukilinganisha na kipindi cha nyuma.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es salaam kwenye uzinduzi wa kampuni ya Visa iliyotambulika kama “Visa Day” ambapo imefungua ofisi nchini Tanzania na itafanya kazi kwa nchi za Afrika Mashariki ambazo ni Tanzania, Burundi ,Uganda na Rwanda .
“Hapo unaweta kuona zamani watu walikuwa wanafanya miamala kwa cash lakini kwa kuwa na Tips ambao gharama zake zipo chini na tips ambayo imeunganisha makampuni yote ya simu tumeweza kuwarahisishia watu walifanya miamala zaidi ya milioni mia tano kwa mwaka mmoja kwa hiyo ni hatu kubwa sana ingawa tunaona sasa hivi watu wanapungua kwenye matumizi ya hundi na cheki lakini tumeona pia miamala kati ya benki moja na nyingine inaenndelea kuongezeka .
“Hata withdraw kwenye ATM zinaongezeka kwa hiyo hata sasa tumeweza kuona baadhi ya maeneo ambayo watu walikuwa wanatumia zaidi cash wameoanza kupunguza zaidi matumizi ya cash wanarudi sasa kwenye matumizi ya simu” Amesema Tutuba
Kwa upande wake Victor Makere Meneja Mkazi wa Visa Nchini Tanzania amesema kuhusu suala la ulinzi wa kifedha wana mfumo maalumu wa kuhakikisha malipo yanapofanyika yanakuwa ni salama hivyo hata malipo ukikosea wana mfumo wanaoweza kuhakikisha unapata fedha zako.