Ujumbe kutoka Benki ya Dunia wakiongozwa na Bi. Gemma Todd wamefika ADEM Bagamoyo kufanya ufuatiliaji wa namna mafunzo ya Utawala Bora wa Elimu kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa yanayoendeshwa kwa Maafisa Elimu Kata nchini yanavyoendeshwa
Wataalamu hao pia wamepata fursa ya kufanya kikao Mkakati na Mtendaji Mkuu Dkt. Maulid J. Maulid ambapo wamejadiliana mambo muhimu kuhusu namna ADEM inavyoweza kunufaika na miradi kutoka Benki ya Dunia hususani uwezeshwaji katika eneo la Kuimarisha Miundombinu ya Mifumo ya TEHAMA itakayosaidia kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi mbalimbali wa elimu nchini.
Vilevile, Wataalamu hao wamepata fursa ya kuzungumza na washiriki wa mafunzo hayo wapatao 246 kutoka Mkoa wa Iringa na Singida na kuwasisitiza kuhusu umuhimu wa kufanya usimamizi fanisi wa shughuli za elimu katika maeneo yao ili kufanikisha malengo ya programu ya BOOST ya kuboresha utoaji elimu ya Awali na Msingi nchini.