Bohari ya Dawa (MSD) Imekutana na wawekezaji, wawakilishi wa makampuni 15 na wafanyabiashara katika sekta ya Dawa na vifaa tiba kwenye ofisi zake zilizopo mkoani Daresalaam.
Wafanyabiashara hao wamefurahi kufika MSD na kupata fursa ya kukutana na kujadiliana na MSD kuhusu fursa mbalimbali za kibiashara na ushirikiano katika nyanja ya ununuzi wa bidhaa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji pamoja na uwekezaji na uzalishaji wa bidhaa za afya.
Akizungumza Mkuu wa ugeni huo Bi. Rekha Sharma kutoka kampuni ya MARS, alisema “Tuna furaha kubwa kuona utayari wa MSD katika uwekezaji hasa kwenye nyanja ya viwanda vya bidhaa za afya. “Tunaamini ushirikiano wetu utachangia kwa kiwango kikubwa katika uzalishaji wa bidhaa muhimu za afya, huku tukikuza ajira na maendeleo ya viwanda”
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Tathmini na Ufuatiliaji wa MSD Hassan Ally alisema “Fursa hii ya ushirikiano inalenga kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha bidhaa za afya zinapatikana kwa wakati, zikiwa na ubora unaokubalika kimataifa, sambamba na kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje na kuchochea ukuaji wa viwanda vya ndani kupitia teknolojia na ajira mpya.”
Mkutano huo ni sehemu ya jitihada za MSD za kuimarisha mnyoMSD roro wa ugavi wa bidhaa za afya kwa kushirikiana na sekta binafsi, hasa kwa kuzalisha bidhaa ndani ya nchi, ili kuhakikisha sekta ya afya inakuwa imara na inayojitegemea aliongeza Hassan.