Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi hiyo wakati wa mafunzo ya udhibiti wa msongo wa mawazo yaliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa Saikolojia na Mahusiano kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Chris Mauki akiwafundisha wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) namna ya kukabiliana na msongo wa mawazo pamoja na kuweka mipaka ya kazi na mambo binafsi. Mafunzo hayo ya siku moja yalifanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakisikiliza mafunzo ya udhibiti wa msongo wa mawazo yaliyokuwa yanatolewa na Mtaalamu wa Saikolojia na Mahusiano kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Chris Mauki. Mafunzo hayo ya siku moja yalifanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.